Breaking News

BENKI YA AKIBA YAZINDUA KAMPENI YA TWENDE KIDIJITALI

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam - Benki ya Akiba imezindua kampeni ya Kidijitali ijulikanayo kama "Twende Kidijitali ili kutoa suluhisho za kifedha.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 18, 2024 na Kitengo cha Masoko na Mawasiliano na kusema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Desemba 12, 2024 jijini Dar es salaam yake mpya ya Twende Kidijitali, inalenga kuboresha uzoefu wa wateja kupitia suluhisho za kifedha za kisasa, za haraka, na za kuaminika. 

Kampeni hiyo inahamasisha matumizi ya huduma za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet Banking, VISA, na Akiba Wakala.

Akizungumza Mkuu wa kitengo cha Biashara wa ACB Dkt Danford Muyango wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,amebainisha kuwa wamejizatiti kuboresha uzoefu wa wateja wao kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Aidha kwa mujibu wa Dkt Muyango kampeni ya "Twende Kidijitali" pia imeungwa mkono na kampeni ya msimu wa sikukuu, "Twende Kidijitali, Tukuvushe January," Lengo la Kampeni:
Kampeni hii ni mwendelezo wa azma ya Akiba Commercial bank Plc ya kuongeza matumizi ya mifumo ya kidijitali ya benki na kuhamasisha wateja kufurahia manufaa ya kutumia teknolojia katika kutatua mahitaji yao ya kifedha.

Kampeni pia inalenga kusaidia wateja kupitia kipindi cha Januari, ambacho mara nyingi kinakuwa kigumu kifedha. Alisema Dkt. Muyango, huku akisisitiza vigezo na masharti ya kampeni hiyo

Aidha ametaja masharti hayo kuwa ni pamoja na Idadi na Thamani ya Miamala ya Kidijitali ambapo Wateja watapimwa kulingana na idadi na thamani ya miamala yao kupitia huduma za kidijitali. 

Pia Wateja walio na ushiriki mkubwa watakuwa na nafasi ya kushinda zawadi kuu za fedha taslimu.
Sharti jingine ni Uzoefu wa Kidijitali na Maoni ya Wateja ambapo Wateja watakaoshiriki kwa kutoa maoni ya thamani kuhusu huduma za kidijitali watapata nafasi ya kushinda katika droo ndogo.

Aidha Wateja watakaowaalika wateja wengine kufanya miamala kwa njia ya ATM, POS, Wakala, Mobile Banking, au Internet Banking, wataweza kushinda zawadi

Alimalizia kwa kusema kuwa, "Benki ya Akiba inawakaribisha wateja wote kushiriki nasi katika safari hii ya kidijitali. Kwa maelezo zaidi, tembelea matawi yetu au angalia majukwaa yetu ya kidijitali.Twendeni Kidijitali na Benki ya Akiba".

No comments