BRELA YAWAJENGEA UWEZO WAHADHIRI UDOM
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), leo tarehe 25 Movemba, 2024 imewajengea uwezo wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) juu ya umuhimu wa usajili wa Alama za Biashara na Huduma na ulinzi wa vumbuzi kupitia Hataza.
Lengo la kuwajengea uwezo ni kuwawezesha wahadhiri pamoja na wanachuo wa UDOM kuweza kulinda bunifu zinazotokana na tafiti zinazofanyika chuoni hapo ziweze kulindwa kisheria na kuwaletea manufaa ya bunifu hizo zilizolindwa. BRELA itatoa mafunzo kwa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi stadi Jijini Dodoma kuanzia tarehe 25 hadi 29 Novemba, 2024.
No comments