Breaking News

RC CHALAMILA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe Albert Chalamila amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dokta Samia Hassan imekuwa ikitoa kipaumbele katika kutunga sera na kuweka Mazingira rafiki na wezeshi kuvutia wawekezaji.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa magari hayo ya kisasa yanayotengenezwa na kampuni ya Kifaru Motors aina ya GWM Tank 500 HEV - Golden Tulip Hotel Masaki amesema kupitia jitihada hizo tayali tumeanza kuona matunda yake kuongezeka kwa uwekezaji na hivyo unatoa fursa za ajira na kukuza uchumi.

"Serikali imekuwa ikijitahidi kuweka Mazingira mazuri na wezeshi kwa lengo la kuvutia wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza hiyo kuongeza fursa za Ajira na kukuza uchumi wa taifa" Alisema Rc Chalamila.

Alisema kupitia maono hayo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan makampuni mbali mbali ikiwemo yanayounganisha magari kutoka ndani na nje
yamekuja kuwekeza katika nchi yetu hususani Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha RC Chalamila ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa hiyo kubwa na yakipekee kupata ajira ambazo zinawawezesha kujikimu kimaisha na kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia ubora wa magari hayo RC Chalamila alisema magari hayo ni mazuri sana yanamuonekano mzuri pia yametengezwa kisasa zaidi kulingana na Mazingira yetu hivyo wananchi wanunue magari hayo.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa Kifaru Motors, Brig Gen Michael Luwongo alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa uzinduzi wa magari hayo ambapo alisema GWM Tank 500 HEV ni gari ya kwanza inayotumia umeme kuanzishwa hapa Tanzania.

"Magari ya GWM 500 Tank HEV pamoja kutengeza magari Bora na kuzingatia azma ya serikali ya kutunzaji Mazingira ni magari ya kwanza ambayo yatakuwa yanatumia nishati ya umeme kuzalishwa nchini". Alisema Brig. Luwongo


No comments