Breaking News

MABINTI 94 WARUDISHWA NCHINI

Jumla ya Wahanga Tisini na Nne wa Usafirishaji Haramu wa Binadamu wamerudishwa nchini kutokea India huku serikali ikitoa wito kwa watu wanaotaka kwenda kufanya kazi nje ya nchi kufuata taratibu ikiwemo kufahamu kampuni wanazoendea kufanyia kazi kama zimesajiliwa kisheria.

Hayo yamesemwa na Afisa Mwandamizi wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Naibu Kamishna wa Jeshi la Magereza, Ahmad Mwendadi wakati wa Semina ya Kupambana na Biashara hiyo iliyotolewa kwa Wawakilishi wa Viongozi wa Mashirika yaliyopo chini ya Umoja wa Wamama Wakuu wa Kanisa Katoliki kutoka mashirika ya Kitawa huku washiriki hao wakiweka wazi umuhimu wa semina hizo katika kupambana na biashara hiyo.




No comments