Breaking News

NAIBU MEYA MANISPAA YA KINONDONI AMJULIA HALI ALLY KALUME, ATOKWA NA MACHOZI

Naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni Michael Urio akitokwa na machozi mara baada ya wakimjulia hali Ally Kalume Ally (41) ambaye amelazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi mapema Leo Agosti 27, 2024

Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
NAIBU Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Michael Urio Leo (Diwani ) amemtembelea na kumlia hali mgonjwa Kalume Ally (41) na kuomba serikali, viongozi wa Serikali kujitokeza kwa wingi kumsadia matibabu na huduma za kibinadamu.

Mgonjwa huyo, Ally Kalume ambaye anasimamiwa kwa ukaribu na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Wa Dar es Salaam (DCPC), amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Kibasila No11,
Awali, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumuona mhe. Urio alisema Kalume yupo kwenye maumivu makali na kuuomba uongozi wa hospitali kumsadia kwa hali na mali.

"Nimefika wodini, nimebahatika kumuona ndugu yetu, kwa kweli yupo kwenye maumivu makali sana, ameniambia na nimemuona, ombi langu kwa uongozi wa hospitali ya Muhimbili tumsaidie ndugu yetu huku sisi tukiendelea kuiomba jamiii imsaidie kwa Hali na Mali, naamini tutafanikiwa" amesema Urio.

Amesema anaomba kutoa wito kwa Mawaziri, Wabunge, Madiwani na watu mbalimbali kujitokeza kumchagia gharama za matibabu.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dk Rachel Mhavile amesema, mgonjwa huyo alipokelewa Agost 24 akitokea Hospitali ya Temeke na tayari ameshafanyiwa vipimo vyote. 

"Tayari ameshachukuliwa vipimo vyote na tunangoja vipimo tuone tunaanzia wapi, kwa Sasa anapewa dawa za kutuliza maumivu , " amesema Dkt. Mhavile kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Dk Mohammed Janabi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamati ya kuratibu matibabu ya Mgonjwa huyo kutoka chama cha waandishi wa Habari mkoa wa Dar es salaam (DCPC), Bi Careen Mgonja ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ukaribu wa Mgonjwa huyo katika kupatiwa matibau huku akiomba wadau na watu mbalimbali kuendelea kuchangia kupitia namba maalum ya aliyeteuliwa.

"Watu wote watakaoguswa kusaidia kuchangia Mgonjwa wanaweza kutuma kiasi chochote cha pesa kupitia kwa Mratibu Mkuu wa zoezi hili, Bi. Kalunde Saidi kupitia namba 0684695698 Jina la mpokeaji likiwa Kalunde Saidi

No comments