Breaking News

MAENDELEO BANK KUWAJENGEA NYUMBA WAMACHINA DSM

Mkurugenzi wa Maendeleo Benki PLC, Dokta Ibrahim Mwangalaba na Makamu Mwenyekiti wa Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) bwana Namoto wakisaini makubaliano ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga wa Mkoa wa Dar Es Salaam katika hafla iliyofanyika Makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo Benki PLC, Dokta Ibrahim Mwangalaba akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga wa Mkoa wa Dar Es Salaam katika hafla iliyofanyika Makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo Benki PLC, Dokta Ibrahim Mwangalaba na Makamu Mwenyekiti wa Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) bwana Namoto Yusuf wakibadilishana mkataba mara baada ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga wa Mkoa wa Dar Es Salaam katika hafla iliyofanyika Makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar Es Salaam.


Dar es salaam:
Maendeleo Benki PLC na Kariakoo Wamachinga Association (KAWASO) wamesaini makubaliano ya kuwapatia mikopo ya gharama nafuu ya ununuzi wa viwanja pamoja na ujenzi wa nyumba za makazi za kisasa kwa wamachinga mkoa wa Dar es salaam. 

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki Plc, Dokta Ibrahim Mwangalaba amesema mradi huo wa kihistoria ambao utaanza rasmi kwa kutoa mikopo ya viwanja utafahamika kama "Machinga plot Finance" tayari hekari 89 zimepatikana katika kijiji cha Magoza wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

"Baada ya kupokea maombi kutoka kwa uongozi KAWASO juu ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo walikubaliana kuanza ununuzi wa viwanja tayari wameshapata hekari 89 katika kijiji cha Magoza wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani" Alisema Dkt. Mwangalaba

Alisema Kupitia mpango huu Bank itatoa mikopo wa zaidi ya Milioni 500 katika awamu ya kwanza ya mradi ili kuwawezesha kumiliki viwanja hivyo ambapo Fedha hizo ni kwaajili ya ununuzi wa ardhi, usafishahi wa eneo husika, upimaji na urasimishaji ili kuwezesha mgawanyo wa viwanja kwa wanachama binafsi na kila mnufaika kuwa na hati miliki ya kiwanja chake.

Dkt. Mwangalaba aliongeza kuwa mpango huo utawawezesha wamachinga wa mkoa wa Dar es salaam kupata viwanja vya bei nafuu kwa malipo isiyozidi milioni moja kwa kiwanja huku wakirejesha kidogokidogo kwa muda wa miezi 12.

Alisema Kukamilika kwa mpango huu, kutawawezesha wamachinga kumiliki ardhi na makazi bora hivyo kuongezea sifa ya kukopesheka zaidi ili kukuza mitaji kutokana na kukidhi sharti la dhamana ya mkopo.

"katika kipindi cha miaka mitatu tumekuwa na mahusiano ya karibu na machinga na kutoa mikopo kwa wamachinga 7,000 zaidi ya Shilingi Bilioni 9.8 ambapo bilioni 7.5 zimerejeshwa na Tzs Bilion 2.3 bado zipo kwa machinga na wanaendelea kulipa" Alisema Mwangalaba.

Mapema makamu Mwenyekiti wa (KAWASSO),Bwana Namoto Yusufu Namoto alianza kwa kuipongeza Maendeleo Benki Plc kwani taasisi nyingi za kifedha nchini zimekuwa zikishindwa kuwahudumia kwasababu mbalimbali lakini leo wote mashahidi makubaliano haya ya kupata mikopo na sasa wanawapa mkopo mkubwa wa viwanja na nyumba.
    
Alisema takribani Masoko 17 yalipo katika jiji la Dar es salaam tayali yameshafikiwa na kupatiwa mkopo kupitia Maendeleo Bank.