OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI KUANZA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MASHAURI YA MAHAKAMA KUU
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Ndg. Mark Mulwambo (aliyeketi kulia) akizungumza na Makatibu Sheria wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akifungua Mafunzo Elekezi kuhusu Matumizi ya Mfumo Mpya wa Mahakama wa Kusajili na Kuratibu Mashauri (e-CMS) yaliyofanyika Mkoani Morogoro. kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masjala ya Sheria Ndg. Dennice Leonard wa Ofisi hiyo.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masjala ya Sheria Ndg. Dennice Leonard wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali akichangia mada kuhusu namna Mfumo Mpya wa Mahakama wa Kusajili na Kuratibu Mashauri (e-CMS) unavyofanya kazi wakati wa mafunzo yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Makatibu Sheria wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wanaoshiriki Mafunzo Elekezi kuhusu Matumizi ya Mfumo Mpya wa Mahakama wa Kusajili na Kuratibu Mashauri (e-CMS) wakifuatilia mada kuhusu namna mfumo huo unavyofanya kazi katika mafunzo hayo yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Ndg. Mark Mulwambo (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Sheria wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mara baada ya kufungua Mafunzo Elekezi kuhusu Matumizi ya Mfumo Mpya wa Mahakama wa Kusajili na Kuratibu Mashauri (e-CMS) yaliyofanyika Mkoani Morogoro. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masjala ya Sheria wa Ofisi hiyo Ndg. Dennice Leonard na wa kwanza kushoto ni Wakili wa Serikali, Bi. Emma Ambonisye.
Post Comment
No comments