Breaking News

TIB YAWEKEZA BILIONI 988.7 KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI NCHINI

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Bi. Lilian Mbasse akifafanua jbo katika kikao kazi kati ya benki hiyo na wahariri wa vyombo vya habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo 16 oktoba jijini Dar es salam

Dar es salaam:
Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) imebaibisha imefanikisha kuwekezaji zaidi bilioni 988 katika miradi mbalimbali ya kimkakati inayoratibiwa na Serikali pamoja na sekta binafsi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na katika kikao kazi kati ya benki hiyo na wahariri wa vyombo vya habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Bi. Lilian Mbasse uwekezaji huo umejikita zaidi katika miradi ya kimkakati hususani nishati, kilimo, madini.

"Benki ya TIB ni benki ya kisera imekuwa ikitoa kifedha katika sekta mbalimbali ikiwemo miradi ya nishati, kilimo, madini, afya, maji na mingineyo". Alisema Bi. Mbise

Alisema asilimia 93 ya uwekezaji miradi ya sekta binafsi na asilimia saba ni katika miradi ya sekta za umma. Wakati asilimia 80 ni miradi ya muda mrefu ambayo inadumu hadi zaidi ya miaka mitano.

Amesema, lengo la kuanzishwa kwa TIB Novemba 1970 ni kujenga Tanzania ya maendeleo ya kiuchumi pamoja na kufadhili msisitizo wa ukuaji wa uchumi wa nchi.

“TIB imekuwa ikitoa mikopo ya muda mrefu na ya kati, na tunafanya hivyo kwa mujibu wa sheria, tukiangalia zaidi katika kuchochea maendeleo, tunaangalia zaidi impact yetu katika maendeleo.” Alisema Bi. Mbise

Akizungumzia Sekta ya Nishati amesema, kuna uwekezaji wa aina mbili. Wa kwanza ni Uwekezaji unajumuisha fedha zao kama benki na aina ya pili ni uwekezaji kupitia fedha za Benki ya Dunia.

“Mpaka kufikia mwezi septemba 2023 TIB imewekeza kwa taasisi kubwa kama TANESCO, shilingi bilioni 12.3 zimetolewa katika nishati. Megawati 8.84 zimezalishwa na kuingizwa katika Gridi ya Taifa.

Amesema TIB imeluwa ikitoa mitaji katika sekta zote nchini ili kuhakikisha ile miradi ambayo inatekelezwa inaleta matokeo chanya kwa ustawi bora wa jamii na uchumi wa Taifa.

Aidha ameongeza kuwa TIB imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kufanikisha miradi ya kimkakati nchini.“Utalii ni miongoni mwa sekta ambazo tunazipa kipaumbele kikubwa. 

Amesema, kuna ajira zaidi ya 30,000 ambazo zinapatikana kulingana na miradi ambayo inafanikishwa na TIB. 

Mbali na kutoa mitaji, TIB pia inatoa huduma ya usimamizi wa mifuko kwa niaba ya wadau wa maendeleo ikiwemo Serikali na wadau wengine. 

Hadi kufikia Septemba 30,2023 wanasimamia mifuko nane. “Sisi kama benki ya kisera, tunatekeleza majukumu yetukwa kuzingatia sera za serikali.”






No comments