DKT. MOLLEL: TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUKATAA UNYANYAPAA KWA WATU WENYE CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI
Na. WAF - Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeitaka jamii kuwekeza zaidi katika afya ya akili kipindi hiki ili kusaidia kukomesha ukiukwaji wa haki za binadamu ambazo watu wenye changamoto za afya ya akili wanaendelea kukumbana nazo siku hadi siku.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa wito huo leo Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani yaliyofanyika Dodoma kitaifa ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu 2023 ni 'Afya ya akili ni haki kwa binadamu wote’.
Ameeleza kuwa Tatizo la Afya ya Akili ni tatizo la kila mtu ili kumaliza tatizo hilo lazima kushikamana kwa pamoja na siyo kuwatenga na kuwanyanyapaa watu wenye changamoto hiyo.
“Lengo kuu la maadhimisho haya ni kujenga na kuongeza ufahamu wa wananchi juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya pombe yaliyokithiri pamoja na kutafakari hali halisi na mwelekeo wa udhibiti wa matumizi haya Kitaifa na Kimataifa, kama tujuavyo matumizi ya pombe yanaleta changamoto kubwa ya uraibu na magonjwa ya akili”. Amebainisha Dkt. Mollel.
Kwa upande wake Bi. Monica Isaya ambae alishawahi kupata changamoto ya Afya ya Akili ametoa rai kwa wananchi kuacha kutumia dawa za kulevya, kutokuwa na msongo wa mawazo pamoja na kujua kufanya jambo gani kwa wakati upi.
“Changamoto hii ya Afya ya Akili inatupata sana sisi wakina mama kwa sababu nyingi ikiwemo kuachwa, kupokonywa mali na watoto pamoja na kujiingiza kwenye mikopo”. Amesema Bi. Monica.
Pia, amesema kuanguka barabarani ambapo unaweza kugongwa na gari na kupelekea ulemavu, kuwa mkali kupitiliza, kutembea bila nguo, kuuwa, kuombaomba, hayo yote ni madhara ya Arya ya Akili.
No comments