Breaking News

MSD YANADI MAFANIKIO YAKE KATIKA SEKTA YA AFYA NA USAMBAZAJI WA VIFAA TIBA NCHINI

Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD) imefanikiwa kuongeza ufanisi katika sekta ya afya usambazaji wa vifaa tiba vya afya kutoka asilimia 51 kwa mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 64 kwa mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD), Bw. Mavere Tukai amesema upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini kwa sasa umefikia asilimia 81

Alisema MSD katika mwaka wa fedha 2022/2 imepokea shilingi bilioni 190.3 ikilinganishwa na sh bilioni 134.9 mwaka wa fedha 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 95.

“Ndugu wahariri haya Ni mafanikio kubwa sana hususani katika utendaji kazi wetu, serikali imetenga bajeti ya kutosha ya kuhakikisha kuwa tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi zaidi" Alisema Bw. Tukai.

Alisema utekelezaji wa Mradi wa Ununuzi na Usambazaji wa vifaa vya huduma kwa wajawazito wanaopata uzazi pingamizi wakati wa kujifungua (CEmONC) ambapo Idadi ya vituo vya kutolea huduma vinavyopelekewa na vilivyopangwa kusambazwa 345, huku Idadi ya vifaa vilivyosambazwa hadi kufikia Juni 2023 ni 299 sawa na asilimia 87.

Bw. Tukai alisema gharama za vifaa vinavyotarajia kusambazwa bil 99.7 wakati thamani ya Vifaa ambavyo vimeshambazwa bil 79.4 sawa na asilimia 80 za utekelezaji.

Amesema MSD imeanzisha kitengo maalumu cha usimamizi na ufuatiliaji wa mikataba jambo lililopelekea kuongezeka kwa ununuzi vifaa tiba vya afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani kuongezeka kutoka bil 14.1 mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia shil bil 39.77

“Bidhaa zinazotoka nje ya nchi ni zile ambazo zinakidhi viwango vya ubora hivyo kutegemena na wazalishaji wa ndani, tumeanzisha zabuni maalumu zinazohusu wazalishaji wa ndani za kuongezea uwezo na ubora wa uzalishaji” Alisema Bw.Tukai.

Alisema ujenzi wa Kiwanda cha mipira ya mikono “gloves” kilichopo Idofi mkoani Njombe umekamilika pamoja na kuendelea kutambua sekta binafsi kwa maeneo ya uwekezaji ya bidhaa za afya za kimkakati za vidonge (tablets), rangi mbili (capsules), vimiminika na bidhaa zitokanazo na zao la pamba na kutangaza matamanio ya ushirikiano kati ya MSD na sekta binafsi

Katika hatua nyengine Bw. Tukai aliongeza kuwa wameboresha ushirikiano na kuongeza ushawishi katika ngazi ya SADC Sekretarieti, na katika ngazi ya Nchi za SADC kupitia balozi zetu

“Tumeimarisha mifumo ya usimamizi kwenye ununuzi na usambazaji wa bidhaa za afya, ushirikiano na wadau wa mnyororo wa ugavi, kushirikisha balozi zetu zilizopo China, Algeria, Urusi na Korea ya Kusini kutafuta wadau wa uzalishaji na ununuzi” Alisema Bw. Tukai.

Alisema MSD tayali imeshaanza kuchukua hatua za kuboresha mifumo ya usimamizi kwa kutumia TEHAMA ikiwemo mfumo wa usimamizi wa magari pamoja na kuanzisha kampuni tanzu itakayoweza kusimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa za afya kwa ufanisi, Ugatuzi wa Utendaji kutoka Makao Makuu kwenda Ofisi za Kanda.

Alisema usimikaji na kuimarisha matumizi ya TEHAMA kwenye ngazi zote za Taasisi, Kutasaidia kuhimarisha matumizi ya takwimu kwenye kazi zote, Kuimarisha mfumo wa usimamizi wa watendaji wa Taasisi na Kuongeza ushirikiano na wazalishaji wa ndani hivyo kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya.

"Uboresha Muundo wa Taasisi utasaidia kuimarisha utendaji wa Taasisi, Ugatuzi wa shughuli zilizofanyika Makao Makuu kwenda Ofisi za Kanda pamoja na Kutumia vyanzo mbadala vya fedha ili kuongezea uwezo wa kifedha Taasisi" Alibainisha bw. Tukai

No comments