Breaking News

KONGAMANO LA KITAIFA LA VIJANA LA URITHI WA UTAMADUNI KUFANYIKA 27 SEPT JIJINI DAR

Asasi ya vijana wa umoja wa mataifa tanzania (YUNA) kwa kushirikiana na makimbusho ha taifa wameandaa kongamano kubwa la kitaifa la vijana juu ya urithi wa utamaduni lifakalofanyika tarehe 26 Septemba katika jumba la makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam.

Kongamano hilo ambalo litawaleta vijana,wadau wa utamaduni watunga sera na wataalam wa utalii litafanyika siku ya kilele cha sikh ya utalii duniani.

Akizungumzia maandalizi ya kongamano hilo mjumbe wa kamati ya uratibu (YUNA) Bi. Irene kigangwa amesema kupitia kongamano hilo vijana watajadiliana kwa tija juu ua umuhimu wa kuhifadhi urithi wetu wa kitamaduni na utalii endelevu.

"Katika kongamano hilo vijana watapata wasaa wa kujadiliana kwa kina juu mambo mbalimbali hususani kuhifadhi uridhi wetu wa kiutamaduni pamoja na utalii endelevu kwa lengo la kukuza utalii endelevu pamoja na kuhifadhi hazina za kiutamaduni" Alisema Bi kigangwa.

Alisema mada mbalimbali zitawasilishwa na wanajopo mashuhuri ikiwemo juu ya ushiriki wa jamii katika uhifadhi wa utamaduni, matumizi ya teknolojia za kidijitali katika uhifadhi wa utamaduni, fursa na changamoto za utalii endelevu katika urithi wa utamaduni.

Kwa upande wake mratibu wa siku ya utalii duniani kutoka asasi ya vijana wa umeoja wa mataifa Tanzania (YUNA) Bwana Greyson Mbugi amesema mkutano huo umelenga kujengea uelewa vijana kuhusu umuhimu wa kuhifadhi urithi wa utamaduni na utalii endelevu na kuwaamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika mipango ya uhifadhi wa urithi wa kitamaduni.

"Kongamano hili lina lengo kubwa la kuhakikisha kuwa vijana wanashiriki kikamilifu katika mipango ya uhifadhi wa urithi wa kitamaduni pamoja na kuongeza idadi ya vijana walioalifiwa kwa lengo la kujitokeza kwa wingi kujitolea kukuza uhifadhi wa urithi wetu wa utamaduni na utalii endelevu" alisema Bw. Mbugi.

Kongamano kitaifa la vijana juu ya urithi wa utamaduni mwaka huu limebeba kaulimbiu ya "Asili yangu Fahari Yangu".

No comments