GST IWEZESHWE - MAGESA
Mbunge wa Jimbo la Busanda mkoani Geita Mhe. Mhandisi Tumaini Magesa ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Madini iiwezeshe zaidi Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili iweze kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini katika kupata taarifa sahihi za uwepo wa madini katika maeneo yao.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 23, 2023 kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofunguliwa na Naibu Waziri Mkuu katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.
Akizungumza juu ya changamoto zinazowakuta wachimbaji wadogo wa madini, Mhe. Magesa amesema kuwa wachimbaji wanafanya kazi za uchimbaji bila kujua sehemu yalipo madini, hivyo kubwa ni vyema serikali iiboreshe Taasisi ya GST ili ifanye tafiti zaidi ili kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini.
Mhe. Magesa aliongeza kuwa jimbo la Busega linawachimbaji wadogo wa madini wengi sana lakini wanachimba kwa kubahatisha na kuharibu mazingira kila siku hivyo Taasisi ya GST ikiwezeshwa itawasaidi wachimbaji kufanya kazi bila kupoteza muda na mitaji yao.
Aidha, Mwenyeti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Nicolaus Kasendamila ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuongeza kasi ya utafiti wa madini ilikuongeza wigo na fursa mbalimbali za upatikanaji wa madini katika mkoa wa Geita.
Maonesho ya Teknolojia ya Madini yalianzishwa mwaka 2018 yakijumuisha kampuni/taasisi mbalimbali zilizo katika mnyororo mzima wa Sekta ya Madini.
No comments