TAS NA LHRC WALAANI MATUKIO YA UDHALILISHAJI WA UTU WA WATU WENYE UALBINO.
Chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) na kituo cha sheria na haki za binadamu wamelaani kitendo kilichofanywa katika kilele cha siku ya simba Day 6 / 8 /2023 kufatia tukio la kumtumia mtu mwenye ualbino akiwa katika hali ya nusu utupu ( kuvalishwa nepi)mbele ya maelfu ya mashabiki katika uwanja wa taifa.
Akisoma tamko hilo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa taifa wa chama cha watu wenye ualbino, Godson Mollel amesema vitendo hivi vinatweza itu wa watu wenye ualbino nchini pamoja na kukiuka katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 12(2).
"Tunalaani tukio hili pamoja na matukio mengine ambalo lilishafanywa na timu hiyo pia mwaka jana 8/ 8 / 2022 siku ya simba day kwa kutumia jeneza na msalaba pamoja na kimnasibu mtu mwenye ualbimo kama msukule" Alisema Bw. mollel.
Alisema vitendo hivi pamoja na kuwa vinautweza utu wa watu wenye ualbino pia vimekuwa vikizua mijadala hususani katika jamii na mitandaoni kufatia kuonyesha dhihaka kwa watu wenye ualbino kinyume na haki za binadamu.
Bw mollel aliongeza kuwa pamoja na jitihada za miaka mingi za utetezi wa watu wenye ualbino nchini katokana na historia ya madhila wanayopitia jambo ambalo limekuwa likipelekea kusababisha idadi kubwa ya wahanga wa vitendo vya ukatili na unyanyapaa.
"Kwa mda mrefu katika jamii nyingi watu wenye ualbino wamekuwa wakihusishwa na mila na tamaduni mbaya zinazotweza utu wao hivyo kushamili kwa vitendo hivi ni kuendelea kudidimiza juhudi za serikali, mashirika watetezi na wadau binafsi za kueleimisha jamii kuhusu ualbino" Alisema Bw Mollel
Kwa upande wake mkurugenzi wa LHRC, Wakili Anna Henda amesema wanatambua utani wa jadi kati ya timu hizo mbili Simba na Yanga bado sio jambo la kuhalalisha vitebdo vya kutweza utu wa mtu kwa sababu yeyote ile iwe kwa kukusudia ama kwakutokukusudia.
Alisema vitendo vya namna hii vinaporuhusiwa kufanywa hususani na taasisi kubwa na yenye ushawishi katika jamii kama timu ya Simba zinarudhisha nyuma jitihada zote zinazochukuliwa kukuza na kuhanasisha taswira chanya.
"Tunalaani kitendo hiki pamoja na vitendo vyote ambavyo vinakiuka na kutweza utu kwani vitendo vya namna hii vinapofabyika tena mbele ya hadhara mbele ya maelfu ya wananchi na kufatiliwa duniani kote ni kurudisha nyuma jitihada zote za kukuza na kuhamasisha taswira chanya ya watu wenye ualbino mbele ya jamii" Alisema wakili Henga.
Aidha wakili Henga ametoa rai kwa taasisi zote hususani zenye ushawishi katika jamii kuepukana na vitendo hivi na kujikita zaidi katika kuhamasisha heshima na utu hususani kwa watu wenye ualbino nchini.
No comments