MWENYEKITI UVCCM DSM NASRA MOHAMED AZINDUA RASMI MASHINDANO YA KOBA CUP, AMPA TANO MWEKEZAJI ASHURA DITOPILE
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es salaam Comrade Nasra Mohammed amezindua rasmi mashindano ya ligi ya mpira wa miguu ya KOBA CUP yalioandaliwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Madenge Mhe. Selemani Koba na Kudhaminiwa na Mkurugenzi wa King Fahad Filling Station ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tawi la Mwasonga Ndg. Ashura Ditopile.
Akizungumza katika kuzindua mashindano hayo, CDE. Nasra ametoa pongezi kwa Mwenyekiti Selemani Koba kwa ubunifu wa mashindano hayo ni kumpongea pia Mwekezaji Ashura Ditopile kwa kudhamini Mashindano hayo ikiwa ni kwa mwaka wa pili mfululizo.
CDE. Nasra amesema jambo hilo ni kuunga mkono moja kwa moja juhudi za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya michezo kwa kuibua vipaji, kuleta Watu pamoja haswa Vijana lakini pia kuwa fursa ya Ajira.
Aidha, CDE. Nasra amewataka Vijana kushiriki michezo hiyo kwa kuzingatia nidhamu, Pia ameahidi kuchangia fedha Tsh 100,000 kwa mchezaji bora wa mashindano hayo.
Pia, Mwenyekiti Selemani Koba ametoa shukrani kwa Mwekezaji Ashura kuendelea kudhamini mashindano hayo na kuwataka Mashabiki kushabikia kwa Furaha na Amani kusiwepo na hali ya kutoelewana.
Aidha, Mwekezaji Ashura Ditopile amesema Mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo atapatiwa Fedha taslimu Tsh 700,000/=, Seti 2 za Jezi, Bips na Mipira 2, Mshindi wa 2 atapatiwa Tsh 400,000/=, Jezi seti 1, Bips na Mpira 1, Mshindi wa 3 atapatiwa Tsh 200,000/=, Jezi Seti 1, Bips na Mpira 1, Pia kutakuwa na zawadi kwa Mfungaji bora na Refa bora.
Aidha, Mwenezi wa CCM (W) Kigamboni Ndg. Abdallah Pazi , Mwenyekiti wa UVCCM (W) Kigamboni Ndg. Amour Gadafi kwa pamoja wameahidi kuchangia katika zawadi za mfungaji bora.
No comments