T-PESA Rasmi Kudhamini BABY Madaha Charity Tour 2021
Shirika la mawasiliano Tanzania kupitia kampuni yake tanzu ya T-PESA wamesaini makubaliano na shirika la Voice of women Organization Kudhamini Baby Madaha Charity Tour.
Akizingumza jijini Dar es salaam mkuu wa kitengo cha masoko bi Dorothy Urio alisema shirika limekuwa likitoa sehemu ya mapato yake kusadia jamii hususani wenye mahitaji maalum.
"Shirika kupitia T-PESA limekuwa likitambua umuhimu wa makundi maalum kwa kutoa sehemu ya faida yake kusaidia shughuli za jamii haswa makundi maalum kupitia tour hii makundi mbalimbali yatanufaika na misaada mbalimbali" Alisema Bi. Urio.
Alisema kupitia Baby Madaha Charity tour ambayo inataraji kufanyika katika mikoa nane pia watatoa misaada na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
Kwa upande wake balozi wa voice of women organization, Baby Madaha alisema ameamua kufanya tour hiyo kwa lengo la kusaidia jamii hususani yenye uhitaji na wanaoishi katka mazingira magumu nchini.
Alisema tour hiyo ambayo imelenga kuamasisha jamii na wasanii kupenda kusaidia wenye uhitaji maalum hususan wanawake na watoto.
Baby Madaha Charity Tour itafanyika katika mikoa 8 kiwepo Dar es salaam, Pwani, Mbeya, Mtwara, Iringa na Dodoma.
No comments