Breaking News

Taasisi ya Hizb Ut Tahriri Yaishauri Serikali Kiangalia Mamlaka Zake za Kisheria

SIKU chache baada ya kuachiwa huru kwa watuhumiwa wa kesi ya ugaidi wa jumuiya ya uamsho wapatao 36 na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP Silvester Mwakitalu ,Taasisi ya Hizb Ut Tahriri  iliyopo jijini Dar es salaam imeiomba serikali kupitia mamlaka zake za sheria  kuwaachia huru watuhumiwa wengine wa makosa kama hayo katika mikoa mbalimbali hapa nchini

Akizungumza na waandishi wa habari mwakilishi kwa vyombo vya habari wa Taasisi hiyo Masoud Msellem alisema kuwa  kuna watuhumiwa wa makosa ya ugaidi kwenye  magereza mbalimbali ya mikoa ya Mtwara,Arusha,Tanga,  pamoja na Dar es salaam hivyo ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali haina budi kuwaachia huru au kusikiliza kesi zao haraka ili haki itendeke.

"kuachiwa kwa washtakiwa hawa thelathini na sita wa ugaidi wa jumuiya ya uamsho ni sehemu ndogo sana ya idadi ya watuhumiwa waliopo mahabusu mpaka sasa ambao wamekaa muda mrefu, kesi zao hazisikilizwi kwa madai kuwa bado upelelezi haujakamilika, tunaziomba mamlaka za kisheria ikiwemo ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kuwachia kwa dhamana watuhumuiwa hao au wasikilize kesi zao haraka" alisema Msellem.

Aidha amesema kuwa sheria ya makosa ya  ugaidi imekua ikilalamikiwa tangu kuanzishwa kwake kwa madai kuwa sheria hiyo inamtaka mtuhumiwa asipewe dhama, akae mahabusu kwa muda ambao haujulikani kulingana na ukomo wa shauri la  upelelezi wa kesi husika lakini pia sheria hiyo haitoi maelekezo kwamba mtuhumiwa akikaa muda mrefu mahabusu halafu akikutwa hana hatia anapaswa kulipwa fidia.

"Hii sheria imekua imekua ikilalamikiwa tangu kuasisiwa kwake na hilo limeendelea kwa muda mrefu kutoka kwa waislam na wasiokua waislama ,sheria hii niya kigeni ya mabeberu,kibaguzi inayolenga kuwakamata na kuwatuhumu kundi fulani ndani ya jamii yaanu wislam,na inapingana na misingi mingi ya haki ikiwemo kumnyima mtuhumiwa dhamana , kumnyima fidia baada yakumuweka mahabusu kwa miaka mingi na mambo mengine" alisema.

Alisema kuwa matumizi ya sheria hiyo yanaharibu mahusiano mema yakijamii kwa kuwa inaleta sura ya wazi kwamba imelenga kuwaonea waislam nakwamba kubwa zaidi sheria hiyo inatoa mwanya kwa watendaji waovu kudhulumu na kuleta uonevu na kutumika vibaya hivyo wameiomba serikali ipitie upya sheria hiyo.

Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na mihadhala ya kiislam wameachiwa huru juni 16 mwaka huu na mwendesha mashkata mkuu wa serikali Dpp Silvester Mwakitalu baada yakusota mahabusu kwa muda mrefu kutokana na tuhuma za ugaidi.
 

No comments