Waraka Wa Maaskofu Kkkt Wajibiwa….Watetezi Wa Rasiliamli Wasio Na Mipaka (Warami) Nao Watoa Waraka
JANA tuliona
katika mitandao ya kijamii waraka wa viongozi wetu wa dini,ukizungumzia masuala
mbali mbali ya nchi na mwelekeo wake huku sehemu kubwa ya waraka huo ukijikita
katika kuikosoa serikali juu ya namna inavyoendeshwa.
Tunafahamu viongozi wa dini wana wajibu wa kiutumishi katika jamii huku
wakilinda dhamira yao ya kuhakikisha umoja wa nchi yetu unabaki kuwa salama kwa
namna yoyote ile.
Inapotokea
mazingira yoyote ya viongozi wetu wa dini kushindwa kusimamia wajibu huo jamii
inayoongozwa na viongozi hao inapaswa ijisimamie yenyewe na kuwakumbusha wajibu
wao huo
Sisi
Watetezi wa Rasiliamli wasio na mipaka (WARAMI) tunaamini kuwa moja wa wajibu
wetu ni kuhakikisha Jamii inapatiwa haki hiyo pasipo upendeleo wa aina
yoyote ule wa kiimani, kisiasa kanda au hata kiukabila
Kwa vyovyote vile
tunaona ni sahihi kwa sasa nasi kupaza sauti yetu kwa jamii ili pamoja na
viongozi wetu hawa wa dini wakiwemo maaskofu wa KKKT tuone ni namna gani bora
ya kuishi katika jamii ambamo watu wake wamechanganyika kwa utofauti
tofauti baina ya dini, kabila, jinsia, ufuasi wa kiitikadi na kadharika
Tunatumia nafasi
hii kuwakumbusha viongozi wetu wa dini wajitafakari kwa umakini na kuanza
kuchagua aina ya maneno ama kauli sambamba na njia wanazotumia ili kutokuleta
taharuki kwa jamii hasa wakizingatia ukweli kwamba mara nyingi sio kila maoni
wanayoona wao yanafaa basi kwetu sisi waumini wao pia yanafaa kwa maana
tuyafuate kama yalivyo.
Miongoni mwa
masuala yaliyoandikwa katika waraka ule wa maaskofu wetu ni malalamiko kuhusu
Katiba Mpya, Uhuru wa kutoa maoni, Usawa katika elimu, mauaji ya watu, uchumi
Demokrasi, kodi kwa wafanyabiashara na ajira kwa vijana kwa kuyataja kwa
uchache.
WARAMI,
tunashangaa ni kwanini waraka huu wa salamu za PASAKA haukujikita zaidi katika
kuwasisitiza waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma
bibilia na maandiko mengine ya dini na badala yake wakajikita katika maoni
yanayong’ata na kupuliza
Watanzania wote ni
mashahidi kuwa kwa sasa nchi yetu imejitanabaisha katika kutatua changamoto
zilizokuwa zinaimbwa kila siku na wanasiasa hasa wa upinzani na kwa kweli
tumeanza kuyaona matunda ya serikali kujikita katika kutatua changamoto hizo
Sote ni mashahidi
kuwa Kuilazimisha Serikali kuitisha mchakato upya wa katiba ni jambo ambalo
haliingii akilini kwa sasa kutokana na ukweli kwamba ni wanasiasa wenyewe
hususan wa vyama vya upinzani ndio waliosusia na kukwamisha mchakato wa katiba
kwa kutaka kulazimisha mawazo yao yawe bila kuzingatia msingi mama wa
Demokrasia kuwa wachache wanasikilizwa wengi wanashinda.
Maaskofu wetu
wamekazana kulalama kuhusu katiba mpya huku waumini wake wanaotuongoza hawana
ufahamu kuhusu BIBILIA
Aidha, tumeona
hivi karibuni namna Rais wa nchi alivyozungumza na jumuiya ya wafanyabiashara
na kuweka wazi changamoto zote zinazowakabili wafanyabiashara ikiwemo suala la
kodi na kuweka mkakati wa pamoja kulitatua, sasa kuendelea kulalamika kwenye
hili hakuna tofauti na nongwa kwa kuwa hata muda alioutoa Rais kwa watendaji
wake haujakwisha.
Maaskofu wetu
wamezungumzia kuhusu utekwaji na mauaji ikiwemo utiaji wa hofu lakini
hawajajikita kuelezea kwa kina hasa ni yepi?,
Sisi tunafahamu
kuwa wapo watu walioathirika moja kwa moja na matukio ya kutekwa na kuteswa kwa
vijana kama Mussa tesha wa Igunga, Joseph yona wa Temeke, Halidi Kagenzi wa
CHADEMA na wengineo yalipaswa kukemewa tangu siku ya kwanza ya kutokea kwake na
si kuyasubiri mpaka leo.
Tunawashangaa
maaskofu wetu hawa kusema kuhusu usawa wa elimu huku wakifahamu kuwa wanamiliki
chuo kikuu ambacho hivi karibuni kilipandisha ada ya masomo na Askofu mkuu
alipoombwa kushusha ada akamwamuru mlinzi afungue geti na anayetaka alipe asome
asiyetaka mlango uko wazi atoke, nafikiri Usawa wa elimu ulipaswa kuanza katika
chuo kinachomilikiwa na KKKT na si vinginevyo.
Maaskofu wetu
wanajaribu kutuaminisha kwamba wao ni wasafi na kila wanachozungumza ni sahihi je
wanadhani wapo wasafi kiasi cha kuwa tayari kuchunguzwa na kuwekwa hadharani
kuhusu Uhalali wa makanisa yao?.
Je maaskofu wetu
hawa ni wasafi kiasi cha kuwa tayari kuchunguzwa matumizi ya mabilioni ya
sadaka wanayokusanya kila siku?.
Ama maaskofu hawa
wanaweza kuueleza umma kuhusiana matumizi ya misaada, misamaha ya kodi
wanayopaswa kulipa na matumizi ya kodi hizo walizosamehewa na serikali.
MAASKOFU WETU
WANATUMIKA?
Hatutaki kuamini
kwamba viongozi wetu hawa wanatumika na wanasiasa kwa maslahi yao ama ya
wanasiasa lakini nafikiri tunapaswa kufikiri sawa kwenye hili kwa kujijibu
maswali machache yafuatayo?
1.
Ikiwa waraka huu wa Maaskofu wetu umesainiwa
tarehe 15-03-2018, kwanini umetoka leo na si kipindi ulipoandaliwa ama siku ya
ibada kama inavyokuwa kawaida ya siku nyingine?
2.
Kwanini waraka huu umetolewa siku moja baada
ya waraka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe ambao kimsingi
maudhui yanafanana kiasi cha kutia shaka kuwa umeandaliwa na mtu mmoja na
maaskofu kushirikishwa kuweka majina yao tu?
3.
Kwanini waraka huu wa Maaskofu
umesambazwa kwa mara ya kwanza na kiongozi wa CHADEMA ambaye pia ni mjumbe wa
kamati kuu wa chama hicho mheshimiwa LEMA ambaye ndiye aliusambaza Waraka wa
Mbowe katika muda unaofanana na njia zinazofanana?.
Ukijijibu maswali
hayo hapo juu unaweza kupata picha halisi
WITO
1.
Tunatoa wito kwa Maaskofu wetu kujikita
katika masuala mahsusi yanayohusu Dini, watuelimishe kwenye dini, wamuachie
Kaisari yaliyo yake nay a Mungu yaliyo yake
2.
Tunawaomba maaskofu wetu wachague njia
sahihi ya kupita kama walivyofanya wenzao waliowatangulia. Wapo viongozi wa
dini walipoona wana wito wa kushiriki Siasa waliamua kuachana Upadri na Uaskofu
na kujikita kwenye siasa.
No comments