Taarifa Za Maandamano Zimemfikia Kamanda Wa Polisi Mkoani Mwanza
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewaonya baadhi ya
watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya
uharifu ikiwemo kuhamasisha maandamano yasiyo halali.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Naibu
Kamishina Ahmed Msangi ametoa onyo hilo hii leo wakati akizungumza na askari
waliokuwa kwenye mazoezi mbalimbali yaliyofanyika katika uwanja wa polisi
Mabatini Jijini Mwanza.
Baadhi ya askari walioshiriki mazoezi hayo
wameeleza kwamba yanawasaidia kuwa imara wakati wote na hivyo kutimiza vyema
majukumu yao.
Kauli hii inakuja baada ya taarifa mbalimbali
kuzagaa mitandaoni zikihamasisha wananchi kufanya maandamano ya amani Aprili 26
mwaka huu, siku ambayo ni Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
ambapo tayari maandamano hayo yamepigwa marufuku na viongozi mbalimbali akiwemo
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Source BMG Media
No comments