SERIKALI Yakiri Kujichanganya Umri Wa Kujiunga Kidato Cha Tano.
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu amefunguka na
kuweka wazi utata ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa kujiunga na masomo ya
kidato cha tano na sita na kusema taarifa ambayo inasambaa imekuwa na makosa.
Semakafu alisema yametokea makosa ya kiuandishi ila kujiunga na masomo ya kidato cha tano
na sita ni miaka 25 na siyo miaka 20 kama ambavyo inasomekana katika taarifa
aliyotolewa jana.
"Kumetokea
makosa ya kiandishi, miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo
inasomeka kwenye ile karatasi" alisema Semakafu
Kufuatia makosa
hayo serikali imetoa waraka mpya kurekebisha ule wa mwanzo, na kipengele cha
miaka 20 wameweka 25.
No comments