Polisi Afariki Baada Ya Kumgonga Mtembea Kwa Miguu
Askari polisi wa
Kituo cha Babati mkoani Manyara, Boniface Masunga (32) amefariki dunia baada ya
baiskeli aliyokuwa akiendesha wakati akielekea kazini kumgonga mtembea kwa
miguu.
Baada ya kumgonga
mtu huyo, askari huo aliangukia kichwa na kufariki dunia papo hapo.
Akizungumza jana
Jumamosi Machi 24, 2018, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Manyara, Agostino Senga
alisema tukio hilo limetokea Ijumaa katika barabara kuu ya Babati-Singida.
Alimtaja
aliyegongwa kuwa ni Awadhi Ashraf (20) mkazi wa mjini Babati na kwamba, chanzo
cha ajali hiyo ni Ashraf ambaye ni fundi ujenzi kuingia barabarani bila
kuchukua tahadhari.
"Huyo fundi
alikuwa anaingia kwenye barabara kuu ya lami bila kuchukua tahadhari, hivyo
akagongwa na baiskeli aliyokuwa anaendesha polisi huyo," alisema Kamanda
Senga.
"Tukio hilo
lililotokea ghafla sana kwani alivyomgonga aliangukia kichwa na kuanza kutokwa
damu masikioni.”
Hata hivyo, baadhi
ya mashuhuda wa ajali hiyo walishangazwa na ajali hiyo kwani hawajawahi kuona
mtu akagongwa na baiskeli na mwendeshaji kufa.
No comments