Taarifa Muhimu:TRL Yasitisha Safari Za Treni19 Na 21 mwezi huu Kwenda Na Kutoka Bara.
Uongozi wa Kampuni ya Reli
Tanzania {TRL) unapenda kuwatangazia wateja wake na wananchi kwa ujumla
kuwa Kampuni inatarajia kufanya marekebisho ya uboreshaji wa miundombinu
ya reli yake katika eneo la kati ya stesheni ya
Morogoro na Mazimbu, ambapo daraja lililopo hapo eneo la km 209/7,
liliharibika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
Daraja
hilo lilisombwa na maji ya mvua mnamo Mei 13, 2017 , majira ya saa 5
usiku na likafanyiwa matengenezo ya dharura tu. Kwa sasa tathmini ya
kiufundi imefanyika na kuthibitisha kuwa ni hatari kuendelea kupitisha
treni hapo bila ya kuliimarisha zaidi.
Uongozi
wa kampuni umeona ni muda muafaka sasa kulifanyia marekebisho madhubuti na ya
uhakika ili kuhakikisha usalama wa wateja wetu na wananchi kuwa unapewa
kipaumbele.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd
Focus Sahani akizungumza na Waandishi Habari makao makuu ya TRL leo asubuhi
kuelezea umuhimu wa ukarabati wa daraja kati ya stesheni za Morogoro na Mazimbu
na hivyo kulazimu kusitishwa safari za treni kwa muda wa siku 2! Pamoja naye ni
Mkuu wa Usalama wa safari za reli Mhandisi Adolphina Ndyetabula kushoto na Mkuu
wa Masoko Nd Shaaban Kiko.
Kwa maana hiyo ili kuweza kuifanya
kazi hiyo kwa umakini Kampuni imefanya marekebisho kidogo ya ratiba yake ili
kutoa nafasi ya kufanikisha zoezi hilo la kulifanyia matengenezo
madhubuti darala hilo.
Hivyo
basi ile treni yetu ya abiria ya siku ya Jumanne tarehe 19 Septemba
2017 kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kigoma na ile treni ya siku ya
Alhamisi ya tarehe 21 Septemba, 2017 ya kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar
es salaam zimefutwa na hazitakuwapo.
Ratiba zetu nyingine zinabakia kama
kawaida hadi hapo tutakapotangaza vinginevyo. Wananchi wanaombwa kuzingatia
hilo na kutuunga mkono ili tuweze kuendelea kutoa huduma zetu kwa uhakika na
usalama unaostahili.
Uongozi wa Kampuni unawaomba radhi abiria na wananchi kwa ujumla
kwa usumbufu utakaojitokeza.
No comments