Jukata Yalaani Vikali Kupigwa Risasi Mhe Tundu Lissu… Watoa Neno Juu Ya Kwamo Wa Katiba Mpya.
Jukwaa la katiba tanzania (JUKATA) limelaani na kusikitishwa na tukio la kupigwa na Risasi kwa mbunge wa singida mashariki na mwenyekiti wa chama cha wanasheria nchini (TLS) Mhe Tundu Lissu lililotokea mjini Dodoma mapema tarehe 7 mwezi huu.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA),
Bw Hebron Mwakagenda alisema kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zilizoripotiwa
juu ya kushambuliwa kwa Mhe Lissu tumesikitishwa na kushangazwa na uonevu
aliofanyiwa mbunge huyo.
“Kwa
mujibu wa taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikiripotiwa na vyombo vya habari
juu ya tukio hilo ni fedheha kwa taifa ambalo linajulikana duniani kote kama
kisiwa cha amani tukio la kumshambulia mtu asiye na hatia kwa risasi zaidi ya
30 sio utamaduni wetu kama taifa” Alisema Bw Mwakagenda.
Alisema
kufatia tukio hilo na mengine mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa nchini kama kuteka,
kuwatesa na kushambuliwa kwa risasi yanayofanywa na watu wasiojulikana
kuendelea kushamili wanatoa wito kwa vyombo vya dola kufanya kazi yake na
wahusika wafikishwe mbele ya sheria.
Pia
JUKATA limeitaka serikali kuchukua hatua za makusudi kukomesha matukio hayo
ambayo yameanza kuota mizizi nchini hivyo kutia doa taifa kutokana miaka mingi kujulikana
kama kisiwa cha amani.
Akizungumzuia
kwamo wa mchakato wa katiba mpya Bw. Mwakagenda alisema JUKATA wamekuwa wakifatilia
na kuzichambua Bajeti ya wizara ya katiba na sheria kwa mwaka fedha (2016/17 na
2017/18) wamebaini serikali aijatenga fedha kwa ajili ya kukamilisha mchakato
huo na wala hakuna maelezo ya kina juu ya hatma ya mchakato huo.
Alisema
pamoja na watumaini ya watanzania walio wengi kuwa mchakato wa katiba mpya
ungeweza kukamilishwa katika kipindi cha kwanza cha utawala wa serikali ya awamu
ya tano chini ya Mhe Dkt. John Pombe magufuli kwasasa yameanza kufifia kutokana
kutotengewa fedha yoyote katika bajeti ya serikali.
Alisema
ikitokea hakuna uwezekano wa kukamilisha mchakatio wa katiba mpya kabla ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kama dalili zinavyo onyesha yafanyike marekebisho
ya msingi ( Minimum Reforms) katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 pamoja na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Alisema
vifungu vya sheria zote zihusuzo uchaguzi vifanyiwe marekebisho hili kuondoa
kasoro ambazo zimekuwa zikilalamikiwa karibu kila uchaguzi ambavyo ni uhuru
kamili wa tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania bara na Zanzibar na Uwezekano wa
kuhoji matokeo ya uchaguzi mahakamani.
Amevitaja
vifungu vingine kuwa ni kuwepo na fursa ya mgombea huru, vyama vya siasa
kuungana, kurejesha mfumo wa ushindi katika uchaguzi wa rais kupatikana kwa kigezo
cha kura zisizopungua asilimia 50.
Pamoja
na kuingizwa katika katiba sheria ya usawa wa kijinsia katika uchaguzi na
katika vyombo mbalimbali vya maamuzi kama mabaraza ya madiwani, bunge na baraza
la wawakilishi.
No comments