Breaking News

Kata Ya Kitunda Kinara Ndoa Za Utotoni Ilala.

Naibu Balozi wa Uholanzi Nchini Bi Juenn Houben akizungumza katika mkutano wa wadau mbambali kujadili mradi wa kuhamasisha jamii kupinga ukeketaji, ndoa za utotoni na ukatili wa jinsia sabamba na uzinduzi wa Tovuti ya shirika la Jukwaa la utu wa mtoto (CDF) jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala Bi. Francisca Makoye akiongea katika mkutano wa wadau mbambali kujadili mradi wa kuhamasisha jamii kupinga ukeketaji, ndoa za utotoni na ukatili wa jinsia sabamba na uzinduzi wa Tovuti ya shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF) jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la jukwaa la utu wa watoto (CDF), Bw.Koshuma Mtengeti akifafanua jambo katika mkutano wa wadau mbambali kujadili mradi wa kuhamasisha jamii kupinga ukeketaji, ndoa za utotoni na ukatili wa jinsia sabamba na uzinduzi wa Tovuti ya shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF) jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi wa shule ya sekondali ya kituda, Gladness Vitus kutoka CDF klabu akielezea namna ambavyo mradi huo una wanufaisha. 
Naibu balozi wa Uholanzi Nchini Bi.Joenn Houben akibonyeza kitufe kuzindua wa Tovuti ya shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF) pembeni yake ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika la jukwaa la utu wa watoto (CDF), Bw.Koshuma Mtengeti jijini Dar es salaam.
Wanafunzi kutoa shule mbalimbali wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.

Dar es Salaam,
Juhudi za pamoja zinaihitajika kati ya serikali na wadau katika kuhakikisha wanachukua hatua za makusudi kutokomeza na kupinga ndoa za utotoni, ukeketaji, mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia.

Wito huo umetolewa mapema leo jijini dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala Bi. Francisca Makoye katika mkutano wadau kujadili mrejesho wa mradi wa kuamasisha Jamii kupinga ukeketaji, Ndoa za utotoni na ukatali wa kijinsia kata ya kitunda.

“Kata ya kitunda ni moja ya kata inayongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha ndoa za utotoni sababu kubwa ni kukithiri kwa ukeketaji wa watoto wa kike hivyo kupitia mradi huu ambao umejikita zaidi kuelimisha jamii juu ya madhara ya ndoa za utotoni, mimba pamoja na mila potofu kama ukeketaji” Alisem Makoye.

Kwa upande wake Naibu balozi wa uholanzi Nchini Bi. Joenn Houben alisema nchi hiyo itaendelea kufadhili miradi mbalimbali ambayo anaamini italeta matokeo chanya katika kutokomeza ndoa za utotoni, mimba, pamoja mila potofu za ukeketaji kwa kuyapatia ufumbuzi.

Alisema vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiwaathiri watoto wa kike kupitia mradi huu jamii itajengewa uelewa hivyo kuwa mstari wa mbele kuhahikisha kuwa watoto hao wa kike wanatambua haki zao na kuzitetea.

Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi mtendaji wa shirika la jukwaa la utu wa watoto (CDF), Bw.Koshuma Mtengeti Alisema mkutano huo ambao umewakutanisha wadau mbalimbali kujadili mrejesho wa shughuli zote zinazoratibiwa na mradi sambamba na kutoa fursa kwa wadau ikiwemo serikali kujadiliana hatua gani ifanyike kutokomeza mila hizo potofu.

Alisema mradi huo umeratibiwa kupitia klabu mashuleni, kuwa na midahalo na watoto pamoja na vijana wa kike na kiume, wanawake na wanaume wa kata ya kitunda kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya athari za ukeketaji.

No comments