ABIRIA WA MABASI YAENDAYO HARAKA KATI YA MBEZI, KIMARA NA MJINI WAMEILALAMIKIA WATOA HUDUMA KUSHINDWA KULETA KADI ZA KIELETRONIKI ZA KUHIFADHI NAULI.
Na Semtawa Jafari
BAADHI
ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendyo haraka kati ya Mbezi, Kimara na
mjini wameilalamikia serikli kwa kitendo chake cha kushindwa kuleta kadi za
kieletroniki ambazo ni maalumu kwa kuhifadhi nauli.
Waliyasema
hayo kwa kwa vile wlizisubiri kadi hizo kwa muda mrefu lakini cha kushangaza
serikali na mtoa huduma wamekuwa wakitoa maelezo ya ambayo hayawaridhishi
abiria hao.
Abiria
hao waliyasema hayo baada ya kubaini kuwa kitendo hicho kinawafanya watumiye
nauli zaidi ya ile iliyopangwa ambayo ni sh. 800 kutoka Mbezi hadi katikati ya
jiji.
Walisema
kutoletwa kadi hizo huenda ikawa ni ujanja wa kutaka kampuni inayotoa huduma
hiyo ujipatia fedha zaiidi kutoka kwa abiria wa wanaoishi Mbezi na ambao hawana
kadi.
Abiria
hao walisema kukosa kwao kadi hizo inawalazimu kulipa sh. 1050 hadi katikati ya
jiji kwa vile wanatakiwa kukata tiketi ya sh 400 hadi Kimara kisha 650 hadi
mjini.
Walisema
wakati kama abiria akiwa na kadi na ikiwa na fedha angetumia sh. 150 hadi Kimara
kisha sh. 650 hadi mjini.
"Kinachoenelea
ni ujanja unaofanywa makusudi ili kuwaibia abiria kwani utaratibu huo unadaiwa
kufurahiwa na kampuni inayotoa huduma hiyo kwa vile unawaingizia fedha nyingi
na ndiyo maana inajitahidi kupeleka magari mengi ili kuwakamata abiria na
kwenda kuwarudika Kimara ambapo wakati mwingine magari yanakuwa machache zaidi
ya abiria,"alilmika mmoja wa abiria hao.
Hata
hivyo, abiria hao walionekana kukata tamaa dhidi ya usafiri huo kutona na
matatizo yake yasiyoisha kila uchao.
No comments