MWAROBAINI WA WA MSONGAMANO WA MBAGALA KUPATIWA UFUMBUZI
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Wilaya za Temeke na Mkuranga
kuangalia namna ya kupunguza msongamano uliopo katika eneo la Mbagala.
Moja
ya hatua alizowashauri kuchukua ni pamoja na kuhamisha kituo cha mabasi ya
mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutoka Temeke hadi Mkuranga.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na viongozi
wa wilaya hizo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafua njia za kuondoa msongamano
huo.
Amesema
kwa sasa hakuna namna ambayo wataweza kuondoa msongamano huo zaidi ya
kuhamishia kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini wilayani Mkuranga.
Waziri
Mkuu amesema eneo la Mbagala kwa sasa lina msongamano mkubwa ambao ni lazima
Serikali ichukue hatua za haraka za kuuondoa.
“Ikiwezekana
mabasi ya mikoa ya kusini yaishie Mkuranga, hivyo kirikianeni kutafuta eneo la kujenga kituo kikubwa cha kisasa cha
mabasi,” amesema.
Amesema
kituo hicho watakachokijenga kiwe na uwezo wa kuhudumia mabasi yote yatokayo
mikoa ya kusini na kituo cha Mbagala kiwe cha daladala za kawaida.
Pia
Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kutawezesha
kuongeza mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.
Aidha
Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kwenda kujadiliana katika vikao vya mabaraza
ya Madiwani juu ya mkakati huo na kisha kumpelekea taarifa ifikapo Februari 15
mwaka huu.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Bw. Filberto Sanga amesema wazo hilo ni
zuri na wilaya yake ina maeneo ya kutosha kujenga miundombinu hiyo.
“Ni
kweli wilaya ya Temeke imeelemewa kwa maana ya maeneo kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu ya maendeleo na haina pa kupumulia zaidi ya Mkuranga , hivyo tupo
tayari kushirikiana nao,” amesema.
Wakati
huo huo, Bw. Sanga ameiomba Serikali itakapoanza awamu ya tatu ya ujenzi wa
mradi wa mabasi ya mwendo kasi ufike hadi Mkuranga mjini badala ya kuishia
Vikindu.
Amesema
kwa sasa wilaya yake ina viwanda 67 ambavyo kati yake vipo vinavyofanya kazi na
vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, hivyo mabasi hayo
yatarahisisha usafiri kwa wafanyakazi.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva amesema amefurahishwa sana na mawazo
hayo ya kuhamisha kituo cha mabasi cha Mbagala kwani katika vitu vilivyokuwa
vinamnyima usingizi ni pamoja na msoingamano wa mabasi na wafanyabiashara
wadogo wadogo katika eneo hilo.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE,
FEBRUARI 7, 2017.
No comments