MGOGORO WA CUF WAZIDI KUSHIKA KASI, MAHARAGANDE HATUNA MPANGO WA KUTAFUTA SULUHU NA PROFESA LIPUMBA.
Chama cha Wananchi
(CUF) kimesema hakitafanya mazungumzo kusaka suluhu na mwenyekiti wake, Profesa
Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kwamba, kipo
tayari kwa lolote hata kama kitafutiwa usajili.
Aidha, chama hicho
kimesema hakijutii kumkaribisha na kumuunga mkono Edward Lowassa, ambaye
aliteuliwa kugombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema na kuwakilisha Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Hayo yamesemwa na Naibu
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF,
Mbarala Maharagande kujibu madai yaliyotolewa na Profesa Lipumba
alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha televisheni hapa nchini.
Katika mahojiano hayo,
Profesa Lipumba alidai kuwa mgogoro uliopo ndani ya chama hicho kwa sasa
hautamalizwa na mahakama pekee bali viongozi wa pande zote mbili wanatakiwa
kuzungumza, lakini Maharagande amesema haiwezekani kwa vile Lipumba
alishakwisha kukivuruga chama na hafai tena kuendelea kuwa kiongozi.
“Lipumba anasema tukae
tulimalize suala hili kwa kuongea sisi wenyewe. Jambo hilo haliwezekani kwa
kuwa kama kupandikiza chuki, uhasama, uharibifu wa chama miongoni mwa wanachama
na viongozi ameshafanya na kufanikiwa hilo kwa baadhi ya wanachama na viongozi wake
na kuharibu taswira ya chama kwa jamii,” amesema Maharagande.
No comments