MHE GODBLESS LEMA ARUDISHWA TENA GEREZANI. BAADA YA SERIKALI KUWASILISHA NOTISI YA KUPINGA DHAMANA YAKE MAHAKAMA YA RUFAA
Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi ya
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga dhamana yake, baada ya mawakili
wa Serikali kuwasilisha notisi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa
wakipinga kusikilizwa kwa rufani hiyo .
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma Maghimbi alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa ya
Jamhuri iliyopinga Lema kupatiwa dhamana
Novemba 11 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha
katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais
John Magufuli, ambapo siku hiyo Jamhuri iliwasilisha notisi ya mdomo.
Baada
ya Lema kufikishwa mahakamani saa 3.25 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali,
huku pia polisi wakiwa wametanda viwanja vya Mahakama Kuu ndani na nje sanjari
na gari moja la maji ya kuwasha, baada ya
mawakili wa pande zote kujitambulisha Jaji Maghimbi alisoma notisi ya
Jamhuri kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa na kueleza kufungwa kisheria
kutoa uamuzi wa rufani hiyo.
No comments