DC APIGA MARUFUKU WALIMU WAKUU KUZUIA KUANDIKISHA WANAFUNZI WASIO NA VYETI VYA KUZALIWA
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu amewapiga marufuku walimu wakuu wa shule za
msingi na sekondari kuzuia kuandikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa
la kwanza hadi wawe na vyeti vya kuzaliwa.
Nkurlu
alitoa agizo hilo baada ya baadhi ya wazazi na wanafunzi kufika ofisini kwake
kusaka vyeti na wengine kulalamika kitendo cha walimu kuwazuia kuanza kidato
cha kwanza.
“Ni
marufuku kwa mwalimu yeyote au kiongozi kuzuia wanafunzi kuandikisha kwa madai
ya cheti cha kuzaliwa kama wanataka kujiridhisha wapate barua kutoka kwa
mwenyekiti wa kitongoji au watendaji wa kijiji na siyo cheti hicho,” alisema
Nkurlu.
Mmoja
wa maofisa elimu kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama, Aruko Lukolela alisema
agizo la mkuu wa wilaya litatekelezwa mara moja.
No comments