BREACHING NEWS: ALIYEKUWA RAIS WA CUBA FIDEL CASTRO AMEFARIKI DUNIA
Aliekuwa Rais wa Cuba fidel castro akiwa na umri wa miaka 90 taarifa za kifo chake zimetangazwa na televisheni ya taifa ya nchi hiyo mapema leo asubuhi.
Fidel Castro wakati wa uhai wake
HISTORI FUPI YA FIDEL CASTRO
Je unamfahamu Fidel Castro? Huyu ni mtu aliyewahi kuwa Rais wa Cuba, mtu ambaye aliwahi kuwa askari wa msituni, mtu ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Kuba naye ni Fidel Alejandro Castro Ruz kwa kirefu
[IMG]
Fidel Castro alizaliwa Agost 13, 1926 ambapo amewahi kuwa mwanasiasa wa Kuba, mwanamapinduzi wa Kuba, Waziri Mkuu wa Kuba kati ya mwaka 1959 hadi mwaka 1976 na amekuwa Rais wa Kuba huru kati ya mwaka 1976 na 2008
Akiwa mwanasiasa wa Kuba Fidel Castro amekuwa amkifuata misimamo mbalimbali ya siasa za ulimwenguni haswa ule wa Marxist na Lenini na baadaye msimamo wa kimapinduzi wa Kuba.
Fidel Casto ameweza kufanya kazi kama katibu wa kwanza wa chama cha Kimkomunisti cha Kuba kati ya mwaka 1961 na 2011, chini ya utawala wake ambao ulikuwa wa chama kimoja, Castro ameweza kusimamia misimamo yake kimataifa.
Fidel Castro ameweza kuwa katibu mkuu wa umoja usiofungamana na upande wowote ule kati ya mwaka 1979 na 1983 na mwaka 2006 na 2008.
Fidel Castro amekuwa akiamini katika kufanya mapinduzi ya mtutu wa bunduki iwe kwa Latino Amerika, Asia na Afrika. “Kuhoji juu ya mapambano ya silaha kuwa ndiyo njia pekee ya ukombozi ninaweza kujibu kuwa ndani ya hoja hii taifa letu hatuna budi, katika raia wengi wa Kuba na mataifa mengi ya latino Amerika, hakuna njia nyingine ya kujikomboa zaidi ya matumizi ya mtutu. Hii inaonekana kuyafaa ata kwa mataifa mengine ya Asia na Afrika.
Kila mara mabeberu wanatumia kila namna wakiyaunganisha majeshi yao kwa kila taifa kuzuia demokrasia ya mapinduzi. Wanawanyonga watu kwa vitanzi, vitanzi hivi vinaweza kukatwa kwa kutumia mapambano ya silaha tu. Wanamapinduzi hawatumii silaha kama njia sahihi ya kujikomboa bali, hii ni njia inayoeleweka wa haraka na wakandamizaji.
Kwa hiyo raia wana njia mbili kuvumilia ukandamizaji au kupambana na adui kwa silaha. Ifahamike wazi kuwa adui huyu ana nguvu za uchumi na kila kitu ata tekinolojia. Mapambano yanajumuisha kutumia kila kitu mlichonacho haswa matumizi ya rasimalia watu.” Anasema Fidel Castro katika mahojiano na mojawapo wa vyombo vya habari akiwa msituni.
Huyo ndiye Fidel Castro, ambaye leo hii amefariki na kuliacha taifa hilo linaongozwa na mdogo wake Raul Castro.
No comments