ATCL YAWATIMUA WA BAADHI YA WAKURUGENZI KUTOKANA NA KUTOKUWA NA VIGEZO VYA ELIMU PAMOJA NA UTENDAJI USIORIDHISHA
Na Joseph Mwalukasa
Shirika la ndege Tanzania(ATCL) limewaondoa katika nafasi zao baadhi ya wakurugenzi na mameneja kutokana na udhaifu wa utendaji wao pamoja na kutokuwa na vigezo vya elimu katika kushika nafasi zao hasa kipindi hiki shirika lipo katika uboreshwaji mkubwa.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi EMMANUEL KOROSSO amesema baadhi ya mameneja hao wameondolewa katika nafasi zao kutokana kuwepo na mapungufu katika utendaji wao kutokana na sababu mbalimmbali moja wapo ikiwa ni pamoja na kutokukidhi vigezo vya kielimu kwa nafasi zao.
Alisema mara baada ya taratibu zote kiofisi zitakapokamilika watapelekwa mikoani kupangiwa kazi nyingine zinazoendana na uwezo wa elimu zao sambamba na kuagiza kuwaondoa wakurugenzi wote waliokuwa wakikaimu nafasi mbalimbali katika shirika hilo na kuwarudisha katika nafasi zao zisizo za kimenijimenti.
Pia katika kuhakikisha shirika hilo linatekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi Mhandisi KOROSSO amemugiza mtendaji mkuu wa shirika hilo kutangaza kazi mara moja nafasi kujaza nafasi zote ambazo zipo wapambamba na kuwaondoa wafanyakazi wote wasio na vigezo na wafanyakazi wasioridhisha katika utendaji.
Kwa upande wa mkurugnezi mtendaji wa shrika la ndege tanzania (ATCL) LADISLAUS MATINDI amesema shiriahilo linakabiliwa na changamoto kubwa ya wataalaumu hasa katika upande wa marubani na wahandisi.
Alisema, kwa sasa shirika hilo lina jumla ya marubani 13 wakati mahitaji ya ndege moja ni marubani 8 hili shirika hilo kujiendesha kwa ufanisi zaidi.
No comments