WACHINA WAKAMATWA MTWARA, WAKUTWA WAKIBADILI EXPIRE DATE KWENYE DAWA
Watu
watano wakiwemo raia wawili wa China na Watanzania watatu wamekamatwa
Mtwara kwa kutuhumiwa kubadili tarehe zilizokwisha muda wa matumizi
kwenye dawa za kilimo (expire date) ili dawa hizo ziingizwe tena sokoni
na kuonekana bado zinafaa kwa matumizi.
Inadaiwa
watuhumiwa hawa wamefanikiwa kubadilisha dawa hizo kwenye mabox zaidi
ya mia sita ( 600) na kuzifanya zionekane mpya ambapo Kamanda wa Polisi
Mtwara amesema Watuhumiwa hao walikamatiwa Nangwanda.
Makachero
wa Polisi baada ya kupewa taarifa waliwahi kwenye eneo la tukio na
kukuta watu wanne wakikwangua chupa kuondoa nembo iliyoonyesha dawa hiyo
ilitengenezwa tarehe 28 February 2013 na muda wake wa matumizi
umekwisha tarehe 27 February 2016.
Nembo
mpya feki waliyoitengeneza Wachina hawa inasomeka dawa imetengenezwa
tarehe 20 February 2016 na inamaliza muda wa matumizi tarehe 19 February
2019.
No comments