Breaking News

RITA KUZIFUTA BODI ZA UDHAMINI ZENYE MAKOSA

Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani) Mara baada ya kupokea ripoti ya  ukaguzi kutoka Taasisi zote zinazofanya usajili wa Asasi za kiraia mapema leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Katiba na Sheria Amon Mpanju.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.


Na Frank Wandiba
Serikali imesema itaendelea kuzikagua na kuzifanyia uhakiki bodi zote zilizo chini ya Wakala wa Ufilisi na udhamini (RITA).

Waziri wa sheria na katiba mhe Harrison Mwakyembe alisema hayo jijini dar es salaam mara baada ya kukabidhiwa Ripoti ya ukaguzi wa taasisi wenye lengo la kuzitambua taasisi zote zilizosajiliwa na kutambuliwa na RITA.

Alisema ripoti hiyo  licha ya kuziorodhesha taasisi ambazo zinatambulika kisheria na kukidhi vigezo, pia ripoti hiyo itazionyesha tasisi ambazo hazikidhi vigezo vya kisheria hivyo kufutwa na kubaki na taasisi zilizosajiliwa na kutambulika kisheria.

Mapema akielezea ripoti hiyo kaimu msajili wa vyama vya kiraia Bi, Marlin Komba alisema taarifa ya bodi ya wadhamini inaonyesha kuwa wadhamini 1944 kati ya 5262 ziliwasilishwa kwa barua pepe (email), huku zingine zikiwasilishwa ofisi.

Alisema kati ya majalada 5262 yaliyowasilishwa majalada 4287 yalichambuliwa na kuwekwa katika kanzi data na kubainika kuwa bodi za wadhamini 500 zilikuwa mfu.

Katika tangazo lililotolewa mei 17 mwaka huu kwenye gazeti la serikali la Daily News pamoja na gazeti la Mwananchi kwa muda wa siku 30, kati ya taasisi 200 ni tasisi 20 tu ndio azikuweza kutekeleza agizo hilo huku taasisi 180 zilibainika kuwa zinatekeleza wajibu.

Aidha ameongeza kuwa taasisi hiyo ina mpango wa kuzifuta taasisi 320 zoezi litakalofanyika mapema mwezi Agost mwaka huu.


 

 
 

No comments