WATANZANIA MILIONI 23 KUPATA NAMBA YA UTAMBULISHO WA VITAMBULISHO VYA URAIA IFIKAPO DESEMBA 31, 2016.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) imeeleza kuwa ifikapo Desemba 31 mwaka huu jumla ya watanzania
milioni 23 watakuwa na namba za utambulisho wa vitambulisho vya Uraia.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami amesema kuwa hatua hiyo ni
utekelezaji wa agizo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Mamlaka
hiyo kuweka saini ya mwombaji na mtoaji wa vitambulisho hivyo.
“Tumeanza kutekeleza agizo la Mhe.
Rais tangu mwezi Juni mwaka huu, hii inamaanisha kwamba vitambulisho
vyote tulivyochapisha kuanzia mwezi Juni mpaka leo vina saini ya
muombaji, saini ya mtoaji na tarehe ya kuzaliwa muombaji” amefafanua
Mdami.
Ameeleza kuwa kazi ya ugawaji wa
vitambulisho hivyo inasubiri kuzinduliwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli atakayekabidhiwa kitambulisho cha uraia namba moja na baadaye
vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wananchi wengine.
Mdami amesema ifikapo Desemba 31
mwaka huu NIDA itakuwa imetoa namba za utambulisho wa vitambulisho hivyo
kwa watanzania milioni 23 kwa kutumia taarifa za Tume ya Uchaguzi
(NEC) zilizo katika vitambulisho vya kupigia kura na kuzihamishia katika
kanzi data ya NIDA.
Amefafanua kuwa ili mwananchi
aweze kupata kitambulisho cha uraia atalazimika kufika katika ofisi za
NIDA akiwa na vielelezo vinavyoonyesha mwaka wake wa kuzaliwa pamoja
udhibitisho wa uraia wake hii ni kutokana na NEC kutokuwa na
viambatanisho hivyo.
Amebainisha kuwa mwananchi mwenye
namba ya utambulisho anaweza kupata huduma zote zinazohitaji namba ya
kitambulisho cha Uraia kutokana na namba hiyo kutobadirika na kuendelea
kutumika hata baada ya kitambulisho kuchapishwa.
Amesema mpaka sasa watanzania
milioni 2.7 wamekwisha patiwa vitambulisho hivyo na milioni 6.5
wamesajiriwa kwa ajili ya kupata vitambulisho hivyo.
Aidha, Vitambulisho hivyo vya
zamani vitaendelea kutumika mpaka utakapotangazwa utaratibu wa
kuvibadirisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vipya.
Pia ametoa ufafanuzi juu ya
malalamiko ya baadhi ya watu wanaodai kwamba wa kumekuwa na mlolongo
mrefu wa kupata vitambulisho hivyo kwa kueleza kuwa NIDA haina namna ya
kufupisha mlolongo huo kwani kufanya hivyo ni sawa na kuuza uraia wa
Tanzania.
Amesisitiza kuwa ni lazima NIDA
ijiridhishe juu ya uhalali na sifa za muombaji ni kuwa ni Mtanzania kwa
kuambatanisha vielelezo vinavyohitajika.
No comments