Breaking News

MAKONDA KUPANDA ULINGONI NA BONDIA CHEKA, 27 AGOST 2016

                                Mkuu wa koa wa dar es salaam mhe Paul Makonda
Bondia Francis Cheka akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya mpambano huo wa kirafiki na mhe mkuu wa mkoa wa dar Paul Makonda wenye lengo la kuamasisha usafi, kulia kwake bi Angelique Moses Afisa kutoka Wrap Fast Food, kushoto kwake Bw Ally Bakari champion mwenyekiti wa waamuzi Tanzania wa TPBC.
Afisa michezo Mkoa wa Dar es salaam Bw Adolph Hahi akifafanua jambo kuhusu mpambano huo wa kirafiki kat mhe mkuu wa mkoa wa dar Paul Makonda na bondia francis Cheka wenye lengo la kuamasisha usafi, kulia kwake bi Angelique Moses Afisa kutoka Wrap Fast Food, kushoto kwake Bw Ally Bakari champion mwenyekiti wa waamuzi Tanzania wa TPBC.
Afisa kutoka Wrap Fast Food ambao ni moja wandaaji Bi Angelique Moses akiongea katika mkutano huo kulia kwake ni Bondia Francis Cheka, kushoto ni Bw Ally Bakari champion mwenyekiti wa waamuzi Tanzania wa TPBC.
Mwenyekiti wa waamuzi Tanzania wa TPBC Bw Ally Bakari akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandalizi ya mpambano huo wa kirafiki.

 Na Frank Wandiba 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe, Paul makonda anatarijiwa kupanda ulingoni 27 agost mwaka huu na bigwa wa masumbwi nchini Francis cheka katika pambano la kirafiki lenye lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira.


Akizungumzia mpambano huo jijini dar es salaam bondia Francis Cheka alisema kupitia kampuni ya ya cheka promotion wameamua kuandaa mpambano huo hili  kihitikia wito uliotolewa na mhe rais John Pombe Magufuli juu ya swala la usafi nchini.


Alisema kupitia pambano hilo kimkakati anayo imani kubwa kuwa atakuwa ameuunga mkono la mhe Rais Magufuli katika uhamasishaji wa usafi wa mazingira zoezi ambalo ufanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi nchini.

Aidha Cheka aliongeza kuwa kampuni yake mara baada ya mpambano huo itaelekea mkoani pia kuhamasisha mabondia kushiriki katika kikamilifu katika zoezi hilo la usafi alisema.

Katika pambano hilo pia kutakuwepo na mapambano ya utangulizi kutoka kwa mabondia wa hapa nchini na nchi jirani.

 



No comments