Mkuu
wa wilaya ya kinondoni mhe ALLY
SALUMU HAPI
Na Frank Wandiba
Katika kutekeleza ahadi ya serikali ya awamu tano ya kutoa elimu
bure kuanzia darasa la awali mpaka
sekondari, wilaya ya kinondoni ilimefanya
uchunguzi na kubaini udanganyifu mkubwa uliofanywa na wakuu wa shule 68 za msingi na
22 za sekondari.
Amekizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam, Mkuu wa
wilaya ya kinondoni mhe ALLY SALUMU HAPI
alisema aliagiza kufanyika kwa uchunguzi hili kutekeleza agizo la mhe
Rais MAGUFULI alilotoa kwa wakuu wa wilaya kuwachukulia hatua kali walimu
wakuu na watendaji wote ambao watafanya udanganyifu na ubadhilfu wa fedha
za elimu bure.
Alisema kufatia agizo hilo aliagiza kufanyika uhakiki wa wanafunzi
darasa kwa darasa na tumebaini
udanganyifu mkubwa, ambapo jumla ya wanafunzi
3,462 wa shule ya msingi na 2,534
sekondari wamebainika kuwa ni hewa na fedha zao azikupaswa kupelekwa.
Baada kugundua udanganyifu huo ofisi yake tayali nimemwagiza mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni awavue
madaraka walimu wakuu 68 wa shule za msingi na 22 wa sekondari.
Aidha mhe HAPI alitoa rai kwa watendaji wengine wa wilaya ya
kinondoni wasio waaminifu na wasiofuata sheria na taratibu kuwa popote walipo
atawasaka na wasipo jirekebisha na kuendana sanjali na kasi ya mhe Rais.
Mwishoni mwa mwezi julai Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr john magufuli alitoa
maagizo kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote nchini kufuatilia kwa
makini fedha za elimu bure hili kubaini udanganyifu na wizi unaofanywa na
watendaji wasio waadilifu.
No comments