Breaking News

SHEIKH JALALA AWATAKA WAISLAM KUYAISHI MEMA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

Waislam wametakiwa kuenzi na kuyaishi yale mema yote aliyokuwa akiyaushi na kusimamia katika kipindi chote uhai wake hili  Kumuenzi Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Akizungumza mapema leo jijini dar es salaam katika Katika Matembezi ya Kumbukumbu ya Kifo cha Mtume MUHAMMAD (s.a.w.w.) kiongozi Mkuu wa Waislam wa dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania, Sheikh Hemed Jalala amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wanatekeleza moja ya mafunzo ambayo alikuwa hakitoa wakati wa uhai wake.

Alisema Mtume Muhammad S.A.W alikuwa kiongozi ambaye alitenda haki na kuwa na huruma kwa watu wote bila ubaguzi hivyo ni jukumu la wanadamu hususani watanzania kujifunza kuishi kwa Amani na upendo Bila kubaguana

"Leo tukiwa tunaadhimisha tukio hili adhimu la kumbukumbu ya kifo cha Kumbukumbu ya Kifo cha Mtume MUHAMMAD (s.a.w.w. yatakayofanyika Tarehe 02/09/2024 sawa na 28/Swafar/1446 Mtume Muhammad S.A.W alikuwa kiongozi ambaye alitenda haki na kuwa na huruma kwa watu wote bila ubaguzi hivyo ni jukumu la wanadamu hususani watanzania kujifunza kuishi kwa Amani na upendo Bila kubaguana" Alisema Sheikh Jalala.

Alisema viongozi wa dini Masheikh, Maimam, wachungaji, maaskofu, mapadre na viongozi wa madhebu mengine ya dini mbalimbali kuondoa tofauti zao hili kujenga umoja na mshikamano na kuiga huruma ya Mtume Muhammad s.a.w. 

Aidha shekh jalala aliongeza kuwa katika Miaka 1400 iliyopita tangu kifo chake  Mtume Muhammad S.A.W alikuwa kiongozi ambaye alitenda haki na kuwa na huruma kwa watu wote bila ubaguzi hivyo ni jukumu la wanadamu hususani watanzania kujifunza kuishi kwa Amani na upendo Bila kubaguana.

Matembezi hayo ya Amani ya kukumbuka kifo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alifariki tarehe 28, Safar, Mwaka wa 11 AH, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania T.I.C, na Hawzat Imam Swadiq a.s yalianzia ilala boma mpaka kigogo post 

No comments