Breaking News

MTANDAO WA KUPINGA RUSHWA YA NGONO WALITAKA BUNGE KUTOPITISHA MAPENDEKEZO YA SHERIA MPYA YA RUSHWA YA NGONO

Mtandao wa kupinga Rushwa ya Ngono wenye jumla ya Mashirika zaidi ya 200 wameomba wabunge kutopitisha mapendekezo ya sheria mpya ya Rushwa ya ngono iliyowasilishwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa TAKIKURU

Mtandao huo umeshangazwa na hatua ya TAKUKURU kukiweka kifungu hicho cha sheria katika muswada huo ambacho kinamlinda muomba Rushwa ya ngono na kumkandamiza aliyeombwa au Muhanga wa Rushwa ya ngono

Wanamtandao huo wanasema Kifungu hicho kina kinachanganya Rushwa ya ngono la biashara ya ngono jambo ambalo nihatari katika kulinda haki za watu kwenye makundi mbalimbali wanaoadhiriwa na Rushwa ya ngono

Mashirika hayo 200 yametoa tamko lao kupinga marekebisho yanayopendekezwa kwenye muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa, hususan kifungu 10 b ambacho marekebisho yake yanahatarisha juudi za Kupambana na rushwa ya ngono kwa kumlenga mwadhirika badala ya kumuwajibisha mhalifu aliyeomba Rushwa hiyo

"Akizungumza na vyombo vya habari, Jijini Dar es Salaam kwaniaba ya wanamtandao huo, Bi Rebecca Gyumi amesema kifungu 10 b kinahalalisha na kuendeleza matumizi mabaya ya mamlaka kwa njia ya kumuhukumu mhanga wa rushwa ya ngono kama mbinu ya kumnyamazisha na kuzima moto wa mapambano dhidi ya rushwa ya ngono" amesena Rebecca

"Tumestushwa sana na hatua hii ya TAKUKURU, lakini tunatuma salamu kwa wabunge, tunawaomba Wabunge wasipitishe sheria hii ambayo itasomwa Bungeni siku ya Jumatatu, tunawakumbusha kuwalinda wasichana na wanawake pamoja na wanaume ambao nao niwahanga wakubwa wa rushwa ya ngono" amesema

No comments