Breaking News

BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA LAWAKUMBUSHA WAGANGA UMUHIMU WA KUZINGATIA SHERIA

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Profesa Hamis Malebo akizungumza katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Tiba ya Mwafrika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Profesa Hamis Malebo  akiteta na Mganga Mkuu wa Jeshi wa Kanda Dkt. Lt. Col. Shabhai.
Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala  Profesa Hamis Malebo  amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuweka kipaumbele na msukumo kwenye kuendeleza tiba asili nchini.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa Hamis Malebo ameyasema hayo katika Kilele cha  maadhimisho  ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika jijini Dar es Salaam Amesema Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala ni chombo cha Serikali kilichoundwa Mwaka 2005 chini ya Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 ya Mwaka 2002, kwa lengo la kusimamia, kudhibiti, kuhamasisha na kuendeleza huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini.

Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu “Kusimamia utoaji wa huduma bora na salama  za Tiba Asili kupitia mifumo sahihi ya udhibiti”.

Amesema salamu za Waganga katika maadhimisho hayo Kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  kuwa ni Mitano  Tena.

Amesema kuwa utafiti wa uwezo wa dawa wameangalia kuwa ni uwepo wa   Bajeti finyu kwa NIMR, Utafiti wa usalama na ubora wa dawa asili GCLA, TBS Vyuo vikuu kwenye Molecules/Viamilifu dawa, preformulation & formulation

Profesa Malebo amesema katika kutimiza majukumu ya msingi ya  Baraza ni  wajibu wa kuendeleza mahusiano baina yake na wadau mbalimbali ili kuhakikisha ufanisi wa huduma za tiba asili na tiba Mbadala nchini.

Aidha katika  jukumu lingine la Baraza ni kusimamia utoaji wa huduma kwa kuwakumbusha waganga umuhimu wa kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo, ili kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma bora na salama.

Aidha amesema  Baraza limepata mafanikio makubwa na ya kujivunia kwa Kusajili wa waganga, dawa na vituo vya kutolea huduma ulianza tangu mwaka 2010 ambapo kufikia mwezi Juni 2024, jumla ya watalaamu 53,499, Vituo vya kutolea huduma 1,758 na Dawa za asili 127 vimesajiliwa kote nchini na kukabidhiwa leseni za kutoa huduma za Tiba Asili na Tiba 
Mbadala.

Hata hivyo amesema udhibiti wa dawa, vituo na matangazo kwa mujibu wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 ya Mwaka 2002, Ibara ya 8(2) Sehemu  4(3)a hadi h, Baraza limekuwa likitimiza jukumu la kudhibiti dawa za asili kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Wizara iliyowaidhinisha na kukasimu majukumu kwa Mamlaka za TMDA, TBS, Maabara ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali, NIMR, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Tiba Asili (MUHAS) kupima dawa asili na kushiriki kama wajumbe wa Kamati ya kusajili dawa asili. 

Ametoa rai rai kwa waganga wa tiba asili kusajili dawa zao Profesa Malebo amesema Baraza linayo miongozo ya udhibiti wa vituo na matangazo.

Amesema katika kuendeleza tiba asili nchini, Baraza limefanikiwa kupata shamba la ekari 126 lililopo Mkoa wa Pwani Wilaya ya Kisarawe katika Kijiji cha Mzenga B kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Ubora wa Tiba Asili pamoja na shamba darasa la miti dawa. 

Profesa Malebo amesema shamba hilo tayari lina Hati ya Kimila na hivyo  Baraza linaomba kupewa fedha kwa ajili ya miradi hiyo ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kupata Hati Milki ya Serikari kwa manufaa endelevu ya tiba asili nchini.

"Baraza linayo furaha kubwa kwa kuwa Wizara ya Afya imeanzisha huduma Jumuishi ya baaadhi ya dawa za asili zilizosajiliwa na Baraza kutumika katika hospitali za rufaa za Mikoa saba  ambayo kwetu ni fursa nchini kwa kukabidhiwa leseni za kutoa huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala" amesema Profesa Malebo.

Amesema kuhusiana na  udhibiti wa dawa, vituo na matangazo, kwa mujibu wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na. 23 ya Mwaka 2002, Ibara ya 8(2) Sehemu 4(3)a hadi h, Baraza limekuwa likitimiza jukumu la kudhibiti dawa za asili kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Wizara iliyowaidhinisha na kukasimu Majukumu mamlaka za TMDA, TBS, Maabara ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali, NIMR, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Tiba Asili (MUHAS) kupima dawa asili na kushiriki kama wajumbe wa Kamati ya kusajili dawa asili.

Amesema katika mikakati Tiba Asili  Serikali iendelee kupanua wigo ili dawa hizo ziweze kutumika katika ngazi zote za vituo vya afya nchini.

Profesa Malebo amesema  changamoto zinazolikabili baraza hilo ni udhibiti mdogo wa dawa za asili jambo ambalo linapelekea matumizi ya dawa zisizo salama au zisizo na ufanisi, Kuwepo na mwamko mdogo katika kusajili dawa asili kutokana na waganga kulalamikia gharama kubwa za upimaji.

Amesema kuna malalamiko ya watengeza dawa za asili wanaopaza sauti kuhusu utaratibu wa kusimamia dawa asili zinazotumika kwenye Huduma Jumuishi. 

Aliongeza kuwa kuna upungufu wa utafiti na ukosefu wa ushahidi wa kisayansi, kuhusu ufanisi na usalama wa dawa za asili na tiba asili kwa ujumla, jambo linalo sababisha  ugumu wa tiba hizi kukubalika na kuunganishwa rasmi katika mfumo wa afya.

Mzozo wa maslahi kati ya tiba za kisasa na tiba za asili unaweza kuzuia ushirikiano na maendeleo.

"Watalaamu wa tiba za kisasa wanaweza kuona tiba asili kama mshindani badala ya kuwa mwenza au mbadala wa matibabu.

Amesema kuna uelewa mdogo kwa jamii na watalaamu wa afya nchini kuhusu tiba asili, jambo linalochangia kutokuaminika na kusababisha  matumizi yasiyo sahihi.

Profesa Malebo amesema baadhi ya watalaam wa tiba asili kujihusisha na imani potofu, jambo linalochangia migogoro na matukio ya kikatili katika jamii, hivyo kushusha hadhi na heshima ya tasinia ya tiba asili

No comments