Breaking News

DAWASA YATANGAZA UWEPO WA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA MIKOA YA DAR ES SALAAM NA PWANI

TAARIFA KWA UMMA

UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA MIKOA YA DAR ES SALAAM NA PWANI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na wananchi wa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani kuwa kumekuwa na upungufu wa huduma ya maji kutokana na hitilafu ya umeme katika mfumo wa kupokea umeme kwenye mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu.

Maeneo yanayoathirika ni maeneo yote  *Mlandizi, Msufini, Vigwaza, Chamakweza, Ruvu, Kwa Mathias, Pangani Bokomnemela, Kibaha, Visiga, Picha ya Ndege, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Makabe, Kimara, Msewe, Changanyikeni, Mabibo, Kisarawe, Ukonga, Kinyerezi, Tabata, Temeke, Segerea, Makuburi, Ubungo Maziwa, Mwananchi, Kiwalani, Lumo, Yombo Vituka, Uwanja wa Ndege, Banana, Viwanda vya Barabara ya Nyerere, Jet, Buguruni, TAZARA.

Wataalam wa DAWASA na TANESCO wanashirikiana ili kurudisha huduma katika hali ya kawaida.

Tunawaomba wananchi wawe wavumilivu wakati Wataalam wanaendelea na jitihadi za kurudisha huduma!

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 
0800110064 (bure) au 
0735 202-121 (WhatsApp tu)

Imetolewa na;
Everlasting Lyaro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA

No comments