WASHINDI WA MASHINDANO YA WAZI YA KUOGELEA TAIFA KUIWAKILISHA NCHI RWANDA NA MAURITIUS
Afisa Michezo Kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) bwana Nicolaus Mihayo akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayofanyika katika bwawa la shule ya kimataifa ya kimataifa ya International School Tanganyika (IST) Masaki Jijini Dar es Salaam.
Dar es salaam
Mashindano ya Wazi ya Taifa ya kuogelea ya siku mbili yamezinduliwa rasmi leo Septemba 23 Katika Bwawa la shule ya kimataifa ya International School Tanganyika (IST) Masaki Jijini Dar es Salaam na yatahitimishwa kesho Septemba 24, 2023.
Akizungumzia katika ufunguzi wa mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) David Mwasyoge amesema lengo ni kutunza dhana ya kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini.
“Lengo la mashindano haya ni kuangalia ‘performance’ ya wachezaji na kutusaidia sambamba na kupata wawakilishi watakaoshiriki mashindano ya Kimataifa,” Alisema Bw. Mwasyoge.
Alisema washiriki watakaofanya vizuri katoka mashindano hayo wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kanda ya Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu nchini Rwanda.
Bw. Mwasyoge aliongeza kuwa washindi hao pia watashiriki pia katika mashindano ya African Junior Championship ambayo yanatarajiwa kufanyika Desemba Mwaka huu nchini Mauritius.
Nae Afisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) bwana Nicolaus Mihayo amesema kama Serikali wapo nyuma ya TSA kuhakikisha wanafanya mashindano yenye ubora.
"Kikubwa na cha Muhimu lengo la mashindano haya ni kupata timu ya zaido ya Wachezaji 40 ambao watakwenda kushiriki mashindano nchini Rwanda," Alisema Bw. Mihayo.
Alisema washindi watapatikana Wachezaji wazuri kupitia mashindano hayo ni imani yake watakwenda kufanya vizuri nchini Rwanda kutakuwa na Wachezaji wa kutosha kushiriki ngazi zote.
Aidha bwana Mihayo pia amevipongeza na kuvishukuru vilabu vyote 14 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara pamoja na Zanzibar kwa kukubali kushiriki mashindano hayo.
Hivi karibuni Mratibu wa Masuala ya Habari TSA Sebastian Kolowa katika taarifa yake aliyoitoa kwa waandishi wa habari kuhusu mashindano hayo, alieleza yatashirikisha vilabu 14 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro pamoja na Zanzibar.
“Mashindano haya ni ya wazi lakini wanaoshiriki ni wale wanachama tu wa Chama cha Kuogelea Tanzania, kwahiyo hata kama kuna mtu anataka kushiriki lakini hayupo klabu yoyote ni ngumu kushiriki,” alisema Kolowa.
No comments