Breaking News

MASHINDANO YA KUOGELEA YA HPT YAFANYIKA JIJINI DAR

Dar es salaam:
Mashindano ya Kuogelea ya HPT awamu ya nne ‘Mixed and Open Swimming Championship’ yamefanyika katika Bwawa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati ufunguzi wa Mashindano hayo Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro ameipongeza HPT kwa kwa kushirikiana na wadai wengine kuandaa mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mafa ya nne nchini.

Mashindano ya mwaka huu na tumeona kweli idadi  ya washiriki imepunguza sana muda ikilinganishwa na mashindano yaliopita lakini napenda kuipongeza HPT kwa kuratibu mashindano ya mwaka huu.

“HPT inaleta vilabu vyote pamoja. Wapo watoto kutoka vilabu vya hapa Dar es Salaam, wengine wanatoka Mwanza, Arusha, Zanzibar na wanakuja hapa kujumuika pamoja na kufanya mazoezi,”Alisema Itatiro.

Alisema washiriki wote  ambao wameshiriki katika mashindano hayo wamekuwa wakifanya mazoezi asubuhi na jioni hivyo kuvunja rekodi (HPT Standard Time).

Aidha Itatiro aliongeza kuwa wao kama TSA wamefarijika sana kwani kupitia mashindano haya wamayo imani kubwa washiriki hata wakipewa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa  watafanya vizuri kitokana na kukidhi viwango vinavyotakiwa.

Nae kocha wa HPT, bwana Michael Livingstone akizungumzamara baafa ya ufunguzi wa mashindano hayo amesema kuwa washiriki wote wamekaa kambini kwa wiki sita jambo ambalo limewafanya watoto kuboresha viwango vyao.

“Hadi sasa katika mashindano haya watoto watano tayali wamevunja rekodi jambo ambalo linaonyesha kuwa viwango vyao vimekuwa na kukidhi hata mashindano ya kimataifa” Alisema Livingstone.

Alisema kufatia ushiriki wa mashindano haya na kulingana na viwango vilivyo onyeshwa na washiriki hivyo kuonyesha wapo tayari kwa mashindano ya Kimataifa





No comments