CUF YAZINDUA SERA YA KIPATO CHA MSINGI NI HAKI YA KILA MTANZANIA
Chama Cha Wananchi CUF kimezindua Sera ya Kipato cha Msingi kwa Wananchi wote (Universal Basic Income) inayolenga kumpunguzia mtanzania, hususan kabwela, ugumu wa maisha.
Sera ya Kipato cha Msingi ni haki ya kila mtanzania ilizinduliwa na Mwenyekiti wa CUF-Chama Cha Wananchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Zakhiem, Mbagala jumapili Agosti 20, 2023. Pamoja na kuizindua Sera hiyo, Prof. Lipumba alizindua pia salamu maalum (Kauli Mbiu) inayosindikiza Sera hiyo: "KIPATO CHA MSINGI NI HAKI YANGU, NI HAKI YAKO".
Sera hiyo iliyopokewa kwa shangwe, bashasha na matumaini mapya na wananchi waliofurika kwenye viwanja hivyo, ilipitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF-Chama Cha Wananchi lililokutana Agosti 17 na 18, 2023 kwenye Ukumbi wa Shaaban Khamis Mloo, Buguruni.
CUF - Chama Cha Wananchi kimeahidi kuifikisha na kuifafanua Sera hiyo ya 'KIPATO CHA MSINGI NI HAKI YA KILA MTANZANIA' nchi nzima.
HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!
Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Agosti 21, 2023
No comments