Breaking News

RC MAKALLA: APIGA MARUFUKU UUZAJI BIDHAA ZA CHAKULA KWA KUZIPANGA CHINI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla kifafanua jambo mara baada ya zoezi la usafi wa pamoja soko la Machinga complex iliyofanyika 28 April 2023 jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla amepiga marufuku utaratibu wa wafanyabiashara kuuza  bidhaa kwa kuzipanga chini hususani bidhaa za chakula kwakuwa ni hatari kiafya hasa msimu huu wa mvua ambapo kunaweza kutokea magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.

RC Makalla ametoa onyo Hilo wakati wa zoezi la usafi wa pamoja soko la Machinga complex ambapo amewaelekeza Viongozi wa masoko yote kudhibiti na kusimamia agizo Hilo.

Aidha RC Makalla ametumia zoezi Hilo kuwahakikishia wafanyabiashara waliokuwa soko la kariakoo kuwa ujenzi ukikamilika kipaombele kitakuwa kwa wale waliokuwepo awali.

Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kupiga marufuku ufanyaji biashara kwenye Maeneo yaliyokatazwa na kuwataka kwenda kwenye masoko rasmi Ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali hususani mikopo.

CPA Makalla pia ameelekeza Kila mtendaji kwenye eneo lake kuhakikisha anasimamia zoezi la usafi na kubainisha kuwa watakaoonekana kulegalega watachukuliwa hatua.




No comments