WAZIRI NAPE: SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUFIKIA UCHUMI WA KIDIJITAL
Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknojia Nape Nauye akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano lililo wakutanisha Wadau wa TEHAMA wa Miundombinu ya Ndani na Nje ya Nchi ‘Connect 2 Connect - C2C’ leo Septemba 7, 2022 Katika hoteli ya serena jijini Dar es salaam.
Washiriki wa kutoka taasisi mbalimbali wakiwasilisha mada katika kongamano la Wadau wa TEHAMA wa Miundombinu ya Ndani na Nje ya Nchi ‘Connect 2 Connect - C2C’ leo Septemba 7, 2022 Katika hoteli ya serena jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Katika kuhakikisha Tanzania inakwenda katika Uchumi wa kidijitali Serikali inatajia kuwasilisha Muswada wa usalama wa Data Mitandaoni katika Bunge linalotajiwa kuanza wiki ijayo.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mara baada ya ufunguzi wa Kongamano lililo wakutanisha Wadau wa TEHAMA wa Miundombinu ya Ndani na Nje ya Nchi ‘Connect 2 Connect - C2C’ leo Septemba 7, 2022, Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknojia Nape Nauye amesema hatua hiyo imetokana kumekuwa na malalamiko kudukuliwa kwa taarifa zao tunataka kulinda taarifa za watumiaji wahuduma kisheria.
"Tunalenga kuwasilisha Mswada wa usalama wa Data Mitandaoni na kulinda huduma za Mitandaoni kwa Misingi ya kisheria". Alisema Waziri Nauye
Alisema serikali kwa kuhaakikisha inatimiza adhma yake ya kuelekea uchumi wa Kidijitali suala la usalama wa Data Mitandaoni ni suala Muhimu.
Aliongeza kuwa Sekta ya Mawasiliano nchini bado imekuwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya miundombinu.
"Serikali imekuwa ikifatilia na kuangalia namna ambavyo unalenga kupunguza Gharama za vifurushi viwe Rafiki kwa watumiaji". Aliongeza Waziri Nape.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA bwana Jabir kuwe bakari amesema serikali imelenga kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Anuwani ya Makaazi.
No comments