MZEE WA U0AKO ATOA KAULI HII KUHUSU TOZO
MCHUNGAJI wa Kanisa la Gospel Rivival Center maarufu kama Mzee wa Upako Anthony Lusekelo amewataka Watanzania kuitumikia nchi yao kwa kuhakikisha wanalipa kodi.
Mzee wa Upako ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam akuzungumza na waandishi wa habiri kuhusu uhusiano uliopo baina ya kodi, tozo na ukristo.
Amesema kuwa nchi yoyote inaendeshwa kwa nguvu za wananchi kwamba suala la ulipaji Kodi na tozo mbalimbali linahistoria ndefu kwani hata katika bibilia limezungumzwa kupitia Taifa la Israeli.
Hata hivyo amesema kwamba wakati wote suala la tozo limekuwa ni mgogoro katika Taifa lolote lakini ameeleza kuwa mbinu ya kuutatua ni kwakuonesha wananchi faida ya kodi au tozo wanazokatwa ikiwemo Ujenzi wa miundombinu ya Afya, maji na kadahalika.
Aidha ameeleza kwamba kwa mataifa yaliyoendelea jambo hili kila mwananchi amekuwa akinivunia kwa kuchangia maendeleo ya Taifa lake lakini sisi tumekuwa ni wagumu katika utoaji Kodi jambo ambalo linapelekea kuundwa kwa sheria na adhabu.
“Wakati wowote Kodi imekuwa ni mgogoro, lakini tozo sio tatizo, tatizo ni namna ya kuutatua mgogoro. Hivyo namna ya kuutatua mgogoro wananchi wanapaswa kuoneshwa faida ya tozo wanazotoa,” amesema Mzee wa Upako Mchungaji Lusekelo.
Kadhalika ametaka wananchi waendelee kupatiwa Elimu ambapo ameeleza kwamba kwa wakristo kutoa tozo ni kuitii Bibilia na maagizo ya Mungu.
Hivyo amewataka Watanzania waipende nchi yao kutoka mayoni na kwa vitendo na sio kupiga kelele tu barabarani na kwamba wawaamini Viongozi wao kwani wapo hapo kwa maslahi mapana ya taifa.
“Naamini Serikali inatoza tozo kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Natoa rai kwa Watanzania wote watoe tozo kwa maendeleo ya Taifa letu,” amesisitiza Mchungaji Lusekelo.
No comments