KAMATI KUU CCCM YAMPONGEZA RAIS SAMIA
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa immpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazozifanya katika kuiletea nchi maendeleo.
Kupitia kikao chake kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam, kamati kuu hiyo pamoja na mambo mengine imesema mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Rais Samia, yanatafsiri kwa vitendo ilani ya uchavuzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema kikao maalum kilichoongozwa na Rais Sami Suluhu kilipokea na kujadili taarifa kutoka vitengo vya chama kuhusu utekelezaji wa kazi za chama na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Shaka, amesema baada ya kujadili kwa kina kamati kuu imefikia maamuzi uamuzi wa kumpongeza Rais Samia kwa namna anavyoendelea kuiongoza ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua hiyo ya kutafsiri kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 –2025.
Pia amehimarisha huduma za kijamii, kuimarisha ustawi wa wananchi, kukuza uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja ikiwa ni kushamirisha na kuharakisha maendeleo endelevu.
Sababu nyingine alizotaja Shaka ni kwamba Rais Samia ametoa kipaumbele katika maeneo muhimu ikiwemo sekta ya Kilimo.
“Bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023, imeweka msukumo mkubwa katika kuboresha kilimo kwa kutenga bajeti kiasi cha shilingi bilioni 954 ikiwa ni ongezeko la asilimia 224.”Amesema Shaka
Amesema fedha katika bajeti hiyo zimeelekezwa katika ruzuku ya mbolea kwa ajili ya kuongeza tija na kushusha bei ya pembejeo kwa wakulima pamoja na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.
“Serikali imetambua kilimo cha kisasa kitaongeza ajira, kitaongeza kipato
cha wakulima, kitaiwezesha nchi kujitosheleza kwa chakula, kitaimarisha uzalishaji na uchumi wa nchi.” Amesema
Amesemam, Kamati Kuu ya CCM, imempongeza pia Rais Samia kwa namna Serikali anayoiongoza ilivyotekeleza na kusimamia zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania imefanikisha Sensahiyo hiyo kidijitali.
Shaka amesema kuwa zoezi hilo la sensa ni msingi muhimu katika kupanga
No comments