Breaking News

WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI ZAIDI YA 100 KUTOKA MISRI WAPANIA KUWEKEZA NCHINI

Waziri ofisi ya waziri mkuu- Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe akiongea na Wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Misri katika hotel ya Hyatt Regency leo 5 December 2021 jijini Dar es salaam.
Naibu waziri wa nishati, Mhe. Steven Byabato akiongea na wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka Tanzania na Misri kwenye mkutano mkubwa uliofanyika Hyatt Regency leo 5 December 2021 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda (Zanzibar) mhem Omar Said Shabani akiongea na Wafanyabiashara na wawekezaji  kutoka nchini Misri na Tanzania katika Hotel ya Hyatt Regency 5 December jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC), Dkt. Maduhu Kazi akifafanua jambo katika mkutano wa wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara kutola nchini Misri mkutano uliofanyika katika hotel ya Hyatt Regency 5 December jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya ELSWEDY, ENG. Ahmed Elsewedy akiongea na Wafanyabiashara na wawekezaji waliofika katika mkutano kati ya Tanzania na Misri katika hotel ya Hyatt Regency 5 Dec 2021 jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kati ya Tanzania na Misri umefanyika hotel ya Hyatt Regency leo tarehe 05 Desemba, 2021 jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huu ulikuwa na lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Misri, kupata taarifa za fursa za uwekezaji zilizopo nchini na vivutio vya uwekezaji. Lakini pia  kukutana na taasisi za Serikali zenye miradi ya kipaumbele ambayo inatafuta wawekezaji.

Mkutano huo umehudhuliwa na Waziri Ofisi ya waziri Mkuu - Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe, Waziri wa Biashara (Zanzibar) Mhe. Omar Said Shaaban, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Steven L. Byabato na Mhe. Mohamed Abdel Wahab Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Misri (GAFI) .

Aidha, kufuatia ugeni huu Kituo cha Uwekezaki (TIC) na Mamlaka ya Uwekezaji (GAFI) wamekubaliana kuanza mara moja utekelezaji Mkataba wa Mashirikiano.  

Ujumbe huo kutoka Misri una wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya 100 ambao pia watashiriki katika uzinduzi wa mradi wa kuzalisha vifaa vya umeme (Electrical Products) wa kampuni ya ELSEWEDY ElECTRIC EAST AFRICA LTD uliopo maeneo ya Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni kesho 6 Desemba, 2021. Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.



Wafanyabiashara, wawekezaji na Viongozi mbalimbali waliofika katika mkutano huo uliofnayika katika hotel ya Hyatt Regency 5 Dec 2021 jijini Dar es salaam.




 

No comments