Breaking News

VIJANA MCHANGAMKIENI FURSA YA KUSOMEA TEKNOLOJIA YA MAJENGO

Timothy Marko
Vijana wametakiwa kujitokeza kusomea tasnia ya ushauri wa kitalamu wa kitenojia katika majengo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza katika Uzinduzi wa bodi ya kitalamu wa kitenojia katika taasisi ya kitenojia  jijini Dar es Salaam, Muhandisi Richard Joseph amesema kumekuwepo na changamoto kubwa ya ujenzi Majengo mbalimbali katika fukwe yasiyokidhi viwango vya kimataifa.
"Kumekuwepo na changamoto kubwa ya ujenzi wa majengo holela pembezoni mwa fukwe bila kuzingatia vigezo na Data ambazo zinatathimini Ubora wa majengo katika nchi za Afrika Mashariki na SADEC".Alisema Muhandisi Joseph.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi na kitengo cha tenknojia DIT, Dkt. Johnson Malisa amesema bodi inao wataalam wa kutosha wanaoweza kutumika katika miradi pamoja kuwajengea uwezo watalamu wa sekta hiyo.

"Bodi inao wataalam wa kutosha na waliobobea ambao wanaweza kutumika kutoa ushauri katika miradi pamoja na kuwajengea uwezo wataalam wanajiunga na sekta hii nchini" Alisema Dkt. Malisa.

No comments