Breaking News

TAHILISO WAMEANDAA TAMASHA KUBWA LA FRESHERS BASH-BATA DEC 10 JIJINI DAR

Jumuiya ya wanafunzi Taasisi za elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) kupitia katiba waliyonayo wamepiga marufuku watu kufanya matukio kwa jina la wanafunzi bila idhini ya jumuiya hiyo atakayebainika akifanya hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake

Angalizo amelitoa leo Jijini Dar es saalam Makamu mwenyekiti wa TAHILISO, Bw Hija Miramba ambapo amesema kumeibuka wimbi la baadhi ya watu kufanya na kushirikisha wanafunzi katika  matamasha yao pasipo kuwashirikia viongozi ambao ni wasemaji mwisho kukitokea matatizo hujiweka pembeni 

Amesema TAHILISO wameamua kuwa wakali kidogo kufatia kushamili kwa matukio hayo ambayo  wamekuwa yakiharibu taswira na muonekano wa wanafunzi kwa kuandaa matamasha ya ajabu ambayo hayabebi hadhi ya wanafunzi

Kwa upande wake Kamishna wa michezo na burudani TAHILISO, Bw. Muba Abduli amesema katika mwaka wa masomo 2021 wameandaa tamasha kubwa linalojulikana kwa jina FRESHERS BASH-BATA litakalofanyika katika viwanja vya posta kijitonyama Desema 10 mwaka huu kiingilio Tsh 10,000 wafunzi wapya na wanafunzi wa zamani wote wanakaribishwa na mtu binafsi.

"Maandalizi ya tamasha hili yanaenda vizuri tayali wasanii mbalimbali wamedhibitisha kushiriki hivyo kutakuwepa na burudani za kutosha pia kutakuwepo na michezo mingine mingi" Alisema bw. Abduli

No comments