Breaking News

RC MAKALA AWATAKA AWATAKA WATENDAJI WA HALMASHAURI ZOTE JIJINI DAR KUSIMAMIA USAFI

Na: Timothy Marko
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amewataka watendaji wa  Halimashauri zote za Mkoa wa Dar es salaam Kuhakikisha zinaimarisha Hali ya usafi katika maeneo Yao.

Akizungumza katika mkutano uliyo wakutanisha wadau wa Makampuni ya usafi mhe. Amosi Makala amesema kuwa lazima watendaji wa manispaa zote wahakikishe wanadhibiti Biashara holela ikiwemo ufanyaji wa Biashara katika Maeneo yasiyo rasmi.

"Lazima mhakikishe Maeneo yote yanakuwa Safi Kwa ngazi ya Kaya na mitaa yenu, sambamba na kudhibiti uchafuzi wa Mazingira na kudhibiti utirishaji wa maji taka."Alisema Mhe. Makala.

Mhe. Makala aliongeza kuwa zoezi la usafi katika jiji la Dar es salaam litaenda sambamba na usafishaji Ukuta pamoja Mitaro, upandaji miti na Bustani.

"Najua Changamoto zenu ikiwemo malipo Kwa wakati Kwa wakandarasi, nimefanya Utafiti wa kutosha Wakurugenzi wahakikishe wanawalipa kwa wakati wakandarasi wenye uwezo na wenye mikataba mirefu". Alisisitiza Makala.
Naye  Muwakilishi wa wakandarasi  wa ukusanyaji wa taka, Azima mkehe akizungumza kwa niaba ya wenzake amehaidi mkuu wa Mkoa watayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa.

No comments